Rais wa Tanzania John Magufuli amewaagiza wakuu wote wa mikoa Tanzania
Bara kuongeza juhudi za utatuzi wa migogoro ya ardhi ikiwa ni pamoja na
kuharakisha mchakato wa kuwanyang’anya hati za umiliki watu wenye
mashamba makubwa ambayo hawayaendelezi.
Rais
Magufuli ametoa agizo hilo leo, Ikulu Jijini Dar es Salaam alipokutana
na kufanya mazungumzo na Wakuu hao wa mikoa, Tanzania ambacho kikao
hicho kimehudhuriwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri
Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe.
George Mcheche Masaju, Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi John Kijazi na
baadhi ya Mawaziri.
“Mashamba yote
yaliyotelekezwa, fuateni taratibu za sheria, yanyang’anyeni wapewe
Watanzania ambao wapo tayari kuyaendeleza, lakini fanyeni jambo hili kwa
kufuata utaratibu,” Rais Magufuli.
Aidha Rais amewaagiza Wakuu wa Mikoa
wote kusimamia kwa ukaribu utekelezaji wa mpango wa ujenzi wa viwanda
katika maeneo yao ili kuwawezesha wananchi kuongeza thamani ya mazao yao
na kuzalisha ajira.
Rais Magufuli amesema kila Mkuu wa Mkoa
anapaswa kufanyia kazi fursa za uanzishaji wa viwanda katika eneo lake
na kuhakikisha anashawishi wawekezaji kuzitumia fursa hizo kama
inavyofanyika katika Mkoa wa Pwani ambako tangu Awamu ya Tano iingie
madarakani viwanda vikubwa 83 vimejengwa na vingine kukamilika huku
viwanda vidogo zaidi ya 120 pia vikiwa vimejengwa
0 MAONI YAKO:
Post a Comment