June 13, 2017

Katika kuunga mkono juhudi za serikali za kuhakikisha benki ya damu nchini inakuwa na akiba ya kutosha, wafanyakazi wa benki ya EXIM wamejitolea damu ili kusaidia wahitaji.
Akizungumza kuhusu utoaji wa damu wa wafanyakazi wa benki ya EXIM, Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali Watu wa benki hiyo, Frederick Kanga amesema ni jambo la kawaida wao kujitolea damu kwani wamekuwa na utaratibu huo kwa muda mrefu na lengo kuisaidia jamii.

 
Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali Watu wa benki ya EXIM, Frederick Kanga.
“Tupo katika utaratibu wa kawaida wa kusaidia jamii, ni utaratibu ambao tumekuwa tukiufanya ni kama asili yetu EXIM kutoa damu kwa mwaka wa saba mfululizo tunajitolea kwa ajili ya kusaidia upatikanaji wa damu kwa wahitaji,
“Tumefikia hatua hii ili kushirikiana na jamii kwa watu wenye uhitaji, tunajitahidi sana kusaidia kwenye sekta ya afya jambo hili huwa linafanyika pia kwenye matawi yetu yote nchini, kwa sasa tunayo 33, 12 yapo hapa Dar na 21 yapo mikoani,” amesema Kanga.
Naye Afisa Uhamasishaji wa Mpango wa Taifa wa Damu Salama Kanda ya Mashariki, Fatuma Mjungu alisema mwitikio wa wananchi kujitolea damu kwa sasa ni mkubwa tofauti na ilivyokuwa awali na muhimu kwa sasa ni utolewaji wa elimu kwa wananchi ili wazidi kutoa kwani bado kuna upungufu mkubwa.

 
Afisa Uhamasishaji wa Mpango wa Taifa wa Damu Salama Kanda ya Mashariki, Fatuma Mjungu.
“Tupo kwenye kampeni ya kuelekea kilele cha siku ya uchangiaji damu kitaifa, tunahitaji kupata chupa za damu 1,500 na mpaka Juni, 12 tulikuwa tumeshapata chupa 735, natoa witio kwa wananchi wajitolee damu kwenye vituo vyetu, changaototo ni elimu sababu wengi wakipata elimu ndiyo wanajitolea,” alisema Mjungu.
 

 



   

  

  

  

 

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE