June 20, 2017

Image may contain: flower 

ZAIDI ya tani 50 za chakula zimetolewa kwa watu wasiojiweza na taasisi ya Khalifa bin Zayed al Nahyan yenye makao yake makuu katika umoja wa falme za kiarabu chini ya usimamizi wa balozi wa falme za kiarabu nchini Tanzania muheshimiwa Abdallah IBRAHIM AL-Suweid.
Zoezi la ugwaji wa msaada huo wa chakula umetolewa kwa wakazi wa mkoa wa Morogoro ambapo jumla ya kaya 832 zimenufaika na msaada huo wa chakula ambao utawawezesha kuweza kupata chakula cha mwezi mzima kwa kaya yenye wastani wa watu wanne.
Vyakula ambavyo vimegawiwa kwa walengwa ni pamoja na unga kilo 25,mchele kilo 20,maharage kilo 10,sukari kilo tano na lita tano za mafuta ya kula.
Akizungumza katika zoezi la ugawaji wa msaada huo kutoka taasisi ya Khalifa bin Zayed al Nahyan, Mwenyekiti wa Taasisi ya The Islamic foundation Al akh Aref Nahdi amesema kuwa jumla ya Tani 54 zimeweza kutolewa kwa watu wasiojiweza katika mkoa wa Morogoro.
Naye katibu mkuu wa taasisi ya the Islamic foundation Sheikh Muhammad Issa amewataka waislamu kuweza kushukuru misaada mbalimbali wanayopatiwa na wahisani ikiwa ni pamoja na kuwaombea dua wale wote wanaowasaidia watu wenye mahitaji.


No automatic alt text available. 

Image may contain: one or more people and crowd

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE