Mkazi wa Kitongoji cha Kazamoyo, wilayani Rufiji, Erick Mwarabu (37) ameuawa kwa kupigwa risasi usiku wa kuamkia leo akiwa nyumbani kwake.
Watu wa karibu katika eneo hilo wamesema
marehemu huyo aliyekuwa askari mgambo alipigwa risasi tatu akiwa
uvunguni mwa kitanda alikokuwa amejificha.
Mkazi mmoja wa eneo hilo
aliyejitambulisha kwa jina moja la Simon amesema watu hao wanaosadikiwa
kuwa ni majambazi walivunja mlango wa nyumba yake saa 9.00 usiku kisha
kuingia ndani na kutekeleza mauaji hayo.
Simon amesema baada ya watu hao kuingia
ndani walipitiliza moja kwa moja hadi kwenye chumba chake ambapo
walimkuta mkewe marehemu na kumhoji alipo mumewe.
Amesema baada ya kuona mkewe hataji
mahali alipo mumewe walianza kumtafuta ndani ya nyumba yake na
kufanikiwa kumuona akiwa amejificha uvunguni mwa kitanda ndipo
wakamfyetulia risasi na kuondoka.
Simon amesema baada ya kutekeleza mauaji hayo hawakuchukua kitu chochote.
Mganga mkuu wa kituo cha afya Ikwiriri, Dk Iddy Malinda amesema
katika uchunguzi walioufanya walibaini marehemu alikuwa na majeraha
matatu ya risasi katika maeneo tofauti ya mwili wake.Dk Malinda amesema mwili huo tayari umekabidhiwa kwa ndugu zake kwa ajili ya mazishi. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Onesmo Lyanga amesema polisi wanaendelea kufuatilia tukio hilo
0 MAONI YAKO:
Post a Comment