Wakati leo Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo na aliyekuwa mgombea wa nafasi ya Rais wa chama hicho mama Anna Elisha Mghirwa akiapishwa na kuwa mkuu wa Mokoa wa Kilimanaro , Kiongozi Mkuu wa ACT na Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe Zuberi ametimkia Ughaibuni
Taarifa hii hapa inasema:
Leo tarehe 06 Juni 2017, Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo Ndugu Zitto Kabwe ameanza safari ya siku kumi kwenda nchi za Uingereza, Ujerumani, Sweden na Denmark kwa safari za kichama.
Madhumuni ya Safari hii, pamoja na kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Chama cha Die Linke cha Ujerumani, ni kufanya mazungumzo na viongozi wa vyama rafiki barani Ulaya ili kuimarisha mahusiano baina ya ACT na vyama hivyo.
Kwa mujibu wa Ibara ya 29(25)(xi) ya Katiba ya ACT Wazalendo, Ndugu Samson Maingu Mwigamba ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kampeni na Uchaguzi ya chama chetu ameteuliwa kuwa Kaimu Kiongozi wa Chama na kufanya shughuli zote za Kiongozi wa Chama katika kipindi chote ambacho Kiongozi wa Chama atakuwa nje ya nchi.
Tunamtakia Ndugu Samson Maingu Mwigamba utekelezaji mwema wa majukumu yake.
Ado Shaibu,
Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mawasiliano kwa Umma,
ACT Wazalendo.
Imetolewa leo tarehe 06 Juni 2017.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment