June 20, 2017

media 

Mgombea urais kupitia muungano wa upinzani nchini Kenya NASA Raila Odinga, ameishutumu serikali kuwatumia wanajeshi na maafisa wa Inteljensia kupanga wizi wa kura kuelekea Uchaguzi Mkuu mwezi Agosti.
Odinga amekishutumu chama cha Jubilee ambacho rais Uhuru Kenyatta ni mgombea wake, kuliingiza jeshi katika siasa za nchi hiyo.
Mgombea huyo ameeleza kuwa ana ushahidi kuwa wanajeshi wanapewa mafunzo katika kambi ya Embakasi jijini Nairobi na mjini Kakamega Magharibi mwa nchi hiyo kupanga namna ya kuingilia Uchaguzi huo.
Aidha, ameonya kuwa kinachotokea ni kama kile kilichojiri mwaka 2007 wakati maafisa wa usalama walipotumiwa kumsaidia Mwai Kibaki kutangazwa mshindi na kuzua machafuko yaliyosababisha vifo vya zaidi ya watu elfu moja.
Amewataka wanajeshi na maafisa wengine wa usalama kutoshawishika na kujiingiza kwenye siasa na badala yake kufanya kazi yao bila kuegemea upande wowote.
“Tunatoa wito kwa wanajeshi wetu, kuwa waaminifu kwa tamaduni za nchi hii na wasikubali kuingilia maswala ya kisiasa,” amesema Odinga.
Hata hivyo, wanasiasa wa Jubilee wamekuwa wakikanusha madai ya Odinga na kusema hayana ukweli wowote.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE