Mwanajeshi wa Somali aliyemuua kwa kumpiga risasi
Waziri mwenye umri mdogo zaidi nchini humo mwezi uliopita, amepewa
adhabu ya kifo.
Waziri Abas Abdullahi Siraji
alikuwa ndani ya gari lake, karibu na Ikulu ya Mogadishu aliposhambuliwa
na mwanajeshi huyo Ahmed Abdullahi Abdi.
Alipohojiwa, mwanajeshi huyo alisema alifikiri kuwa Waziri huyo alikuwa gaidi na kuamua kumpiga risasi.
Mahakama ya kijeshi iliyotoa adhabu hiyo imesema mwanajeshi huyo anaweza kukata rufaa.
Somalia bado inatekeleza adhabu na kifo kwa kupigwa risasi hadharani na kikosi maalum.
Maafisa wa juu wa serikalini nchini humo hulindwa na idadi kubwa ya walinzi waliojihami kwa silaha nzito kwa hofu ya kushambuliwa na kundi la Al Shabab.

0 MAONI YAKO:
Post a Comment