KIUNGO
wa kimataifa wa Rwanda, Haruna Hakizimana Fadhil Niyonzima, amesema
yeye bado ni mchezaji wa Yanga na hajasaini kwa mahasimu Simba kama
inavyovumishwa.
Akizungumza
na Bin Zubeiry Sports – Online leo mchana, Niyonzima amesema kwamba
anastaajabishwa na uvumi kwamba yeye amesaini Simba, wakati si kweli.
Pamoja
na hayo, Niyonzima amekiri kufanya mazungumzo na viongozi wa Simba,
lakini hajafikia hata makubaliano ya kusaini zaidi ya kuwasikiliza tu na
ofa yao.Haruna Niyonzima amesema yeye bado ni mchezaji wa Yanga na hajasaini kwa mahasimu Simba kama inavyovumishwa
“Nipo kwenye likizo, nimeelekeza fikra zangu kwenye mambo ya familia zaidi kwa kipindi hiki, pili mimi naamini kama ningekuwa nimesaini huko (Simba), au nimesaini huku (Yanga) kila mtu angejua, hivyo kwa sasa sijasaini timu yoyote,”amesema. Haruna amesema kwa sasa anasikiliza ofa mbalimbali zinazoletwa kwake, kabla ya kuamua asaini wapi. “Mimi kama mfanyabiashara naweza nikaongea na timu yoyote, haya yanayoendelea sasa yataisha,”amesema. Mzaliwa huyo wa Gisenyi, Rwanda Februari 5, mwaka 1990 alijiunga na Yanga SC mwaka 2011, akitokea APR ya Rwanda aliyoanza kuichezea mwaka 2007 baada ya kujiunga nayo kutoka Rayon Sport iliyomsajili mwaka 2006 kutoka Etincelles iliyomuibua kisoka nchini humo.

0 MAONI YAKO:
Post a Comment