June 19, 2017

 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli anatarajiwa kuzindua viwanda vitano kesho tarehe 20 Juni, 2017  Mkoa wa Pwani. 

 
Taarifa kutoka Ikulu imesema kwamba Rais Magufuli anategemea kuanza ziara ya siku tatu ambapo miradi mbalimbali itazinduliwa ikiwa ni pamoja na mradi wa maji, barabara ya Bagamoyo – Msata. na viwanda.
Viwanda vikubwa vitano ambavyo vitazinduliwa ni pamoja na kiwanda cha vifungashio (Global Packaging Co. Ltd), kiwanda cha matrekta (Ursus-TAMCO Co. Ltd), kiwanda cha chuma (Kiluwa Steel Group), kiwanda cha kukausha matunda (Elven Agric Company) na atafungua kiwanda cha vinywaji baridi (Sayona Fruits).
Aidha, katika ziara hiyo Mhe. Rais Magufuli atakutana na kuzungumza na wananchi katika mikutano ya hadhara iliyoandaliwa.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE