Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU, imewapandisha
kizimbani watu wawili James Rugemalila na Harbinder Seth Sigh kwa tuhuma
ya kesi ya Uhujumu Uchumi Katika sakata la ESCROW NA IPTL baada
yakufanyika kwa uchunguzi wa muda mrefu.
Watuhumiwa
hao ni Mmiliki wa kampuni ya VIP Engineering and Marketing, James
Rugemalira na Mmiliki wa Kampuni ya kufua umeme ya Independent Power
Tanzania Ltd IPTL, Habirnder Seth mwenye asili ya bara la ASIA
wamesomewa mashtaka sita ya uhujumu uchumi katika mahakama ya kisutu
jijini Dar es Salaam.
Akisoma mashtaka mbele ya mwendesha
mashtaka Poul Kadushi, Wakili wa PCCB Joseph Ihula amesema, mnamo tarehe
18 Octoba mwaka 2011 na tarehe 19 March 2014 matika maeneo mbalimbali
nchini Tanzania, Kenya, Afrika kusini na India watuhumiwa hao walitenda
kosa la kufanya udanganyifu na kujipatia pesa Katika, shtaka la pili
watuhumiwa hao wanakabiliwa na kosa la kujihusisha na uhalifu kwa
kushirikiana na baadhi ya watumishi wa umma, na shtaka la tatu na la nne
yanayomkabili mtuhumiwa wa kwanza Habirnder Seth ni pamoja na kugushi
cheti cha usajili na kutoa nyaraka za kugushi kwa msajili wa makampuni.
Shtaka la 4 na 5 yanayo wakabili
watuhumiwa wote wawili nikujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu kiasi
cha zaidi ya Dola za kimarekani Milioni 22 na kiasi kingine cha pesa za
kitanzania Bilioni 309 za kitanzania pamoja na kuisababishia serikali
hasara ya kisi cha Bilioni 309 za kitanzania.
Upelelezi wa shtaka hilo haujakamilika
na watuhumiwa wote wamerudishwa mahabusu ambapo kesi yao itatajwa tena
tarehe tatu mwezi wa saba mahakamani hapo.
Awali kabla watuhumiwa hao kupandishwa
kizimbani, Mkurugenzi wa TAKUKURU Bwana Valentino Mlowola amewaambia
waandishi wa habari kuwa mara baada ya kukamilika kwa taratibu za
kimahakama kesi hiyo itahamishiwa katika mahakama ya kushugulikia makosa
ya uhujumu uchumi maarufu kama mahakama ya mafisadi.
"Leo tunawapa taarifa kwamba
tunawafikisha Mahakamani watuhumiwa wawili bwana Harbinder Singh Sethi
na James Rugemalila na hawa tuna wafikisha Mahakamani kwa kosa la
uhujumu uchumi na makosa mengine yanayo hayo kwa muda mrefu sana nimekua
naulizwa kesi za ESCROW na IPTL imeishia wapi, kama tulivyosema mwanzo
kwa Taasisi ya Kuzuia na kupambana na kuzuia rushwa na makosa ya
ufisadi,” alisema Mlowola.
Aidha Bw. Mlowola ameongeza kwamba “Nataka
nitoe wito kwa Watanzania kwamba serikali ina nia nzuri na dhati ya
vitendo vya kuhujumu uchumi wa nchi yetu ili wananchi wapate maisha bora
zaidi na jukumu hili TAKUKURU tutaendelea kulitekeleza kwa nguvu zetu
zote kwa weledi wetu wote na kwa umakini wa hali ya juu na kuhakikisha
kwamba vitendo vyote vya kuhujumu uchumi vinadhibitiwa ili wananchi
wapate maisha bora”.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment