Assalam Alaykum warahmatullah Taara wabarakatu. Tukiwa tunaelekea kumaliza mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhwani. Moja ya masharti ya funga ni kuzitolea funga zetu Zakaatul-Fitwr ili zipate kutwaalika mbele ya Allah. Kabla ya kufikia mwisho wa Ramadhani basi tunaomba tukumbushane baadhi ya masharti ya Zakaatul-Fitwr
Hairuhusiwi Kumpa Zakaatul-Fitwr Mtu Ambaye Umewajibika Kumuhudumia
SWALI
Mimi
mwanamke nnayeishi nchi za nje. Nimeolewa nikiwa na watoto saba. Kila
mwaka nampelekea mama yangu Zakaatul-Fitwr ambaye anaishi Tanzania, nami
ndiye nnayemhudumia kwa mahitajio yake (mwenye mas-uliya naye). Je,
naruhusiwa kumpa Zakaah au haifai?
JIBU:
Sifa Zote Ni Za Allaah
Maulamaa
wamekubaliana bila ya kukhitilafiana kwamba hairuhusiwi kutuma Zakaah
ya fardhi ambayo inajumuuisha Zakaatul-Fitwr kwa mtu ambaye inampasa
kumhudumia (kuwa na mas-uliya nao) kama wazazi na watoto.
Inasema katika al-Mudawaanah (1/344):
Je, Vipi kuhusu Zakaah ya mali, kutokana na rai ya Maalik nimpe nani?
Akajibu:
"Usimpe yeyote katika jamaa zako ambaye unapaswa kumhudumia" [mwisho wa kunukuu]
ash-Shaafi'iy kasema katika al-Umm (2/87)
"Asimpe (Zakaah ya mali) baba yake, mama, babu au bibi" [mwisho wa kunukuu]
Ibn Qudaamah kasema katika al-Mughniy (2/509):
“Zakaah
yoyote ya fardhi isitolewe kwa wazazi hata mstari (wa ukoo) ukifikia
vipi (yaani mababu na mabibi) au watoto hata mstari (wa ukoo) ukifikia
vipi (yaani wajukuu).”
Ibn Mundhir kasema:
"Maulamaa
wamekubaliana bila ya kukhitilafiana kwamba hairuhusiwi kuwapa Zakaah
wazazi ikiwa hali ya mtoaji ni mwenye kuwahudumia kwa sababu kuwapa
Zakaah kutamaanisha kuwa hawahitaji tena awahudumie na manufaa yake
yatamrudia yeye. Hivyo ni kama kujipa mwenyewe (hiyo Zakaah) nayo hairuhusiwi. Hali hiyo kadhalika ingelikuwa kama kujilipia deni lake mwenye" [mwisho wa kunukuu]
Shaykh Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah) aliulizwa kuhusu hukmu ya kumpa Zakaatul-Fitwr jamaa ambaye ni masikini:
Akajibu:
"Inaruhusiwa kumpa Zakaatul-Fitwr na Zakaah ya mali ya mtu kwa jamaa ambao ni maskini. Bali
kuwapa jamaa ni bora kuliko kuwapa watu wageni kwa sababu kuwapa jamaa
ni sadaka na pia kuunga ukoo. Lakini sharti kwamba kuwapa sio kwa
kuhifadhi mali
yake mtu, yaani ikiwa huyo jamaa masikini ni ambaye anapasa kumhudumia.
Katika hali hii, hairuhisiwi kumtimizia haja zake kwa kumpa Zakaah kwa
sababu akifanya hivyo atakuwa amehifadhi pesa zake mwenyewe kwa kumpa
yeye Zakaah na hivyo hairuhusiwi. Lakini ikiwa hana mas-uliya naye ya
kumhudumia basi anaweza kumpa Zakaah yake, na kumpa Zakaah yake ni bora
kuliko kumpa mtu mgeni kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Sadaka yenu kwa jamaa ni sadaka na pia kuunga ukoo)) [mwisho wa kunukuu]
Kwa hiyo, hairuhusiwi kwako kuitoa Zakaatul-Fitwr yako kumpa mama yako, bali umhudumie kutokana na mali yako nyingine isiyokuwa ya Zakaah. Na tunamuomba Allaah Akuruzuku rizki kwa wingi"
Na Allaah Anajua zaidi
0 MAONI YAKO:
Post a Comment