Saida ambaye kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake mpya Orugambo,
amesema hit song ya Darassa ‘Muziki’ ni vigumu kuja kushuka na kuwataka
wasanii wengine hasa wa hip hop kuchukulia hilo kama somo.
“Wimbo wa Darassa utaendelea kuhit, utaendelea kuwa shule kwa
waimbaji wa hip hop. Nitapenda watumie akili alizotumia Darassa, mimi
naamini wimbo wa Darassa hauwezi kushuka hata siku moja na Watanzania
wengi walikuwa hawapendi muziki wa hip hop lakini Darassa kuonyesha njia
kwa sababu sasa hivi hadi kwenye harusi wanaimba acha maneno weka
muziki, hadi Bungeni,” Saida ameiambia Clouds FM.
Kwa upande wa Ray C Saida amesema licha ya msanii huyo kupitia
matatizo mengi bado uwezo wake upo pale pale na kuna baadhi wamejaribu
kumuiga ila wameshindwa.
“Kwa kweli Ray C nampenda sana kutoka moyoni tangu zamani, sauti yake
ni nzuri haina mpinzania, wasichana wengi wamejaribu kuiga kuimba kama
yeye, wanapenda mvuto wake na muonekano wake lakini wameshindwa,”
amesema Saida na kuongeza.
“Na ukiangalia Ray C amepitia matatizo makubwa sana hapa katikati
lakini napenda kumshukuru Rais Mstaafu Mheshimiwa Jakaya Kikwete
alipomsaidia Ray C, na ningependa Rais wetu wa sasa, Dkt. John Magufuli
afanye hivyo ili tuweze kunyanyuka sisi tuliokwama,” ameeleza Saida.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment