June 11, 2017

Ndoa za watu wa jinsia moja zilifanywa kuwa halali nchini Marekani miaka miwili iliyopita 

Maelfu ya watu wameandamana katika kile wanachokiita kudai haki za watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja mjini Washington, nchini Marekani.
Yanatajwa kuwa maandamano makubwa kuwahi kushuhudiwa tokea kuingia madarakani kwa Trump.
Wengi wao wanadai kuwa wanapata vitisho na hawajui mustakabali juu ya maisha yao.
Ndoa za watu wa jinsia moja zilifanywa kuwa halali nchini Marekani miaka miwili iliyopita, lakini watetezi wa haki za binaadam wanasema bado wanatengwa katika masuala kama ajira.
Maandamano haya yamekuja karibia mwaka mmoja baada ya watu 49 kuuawa kwa kupigwa risasi kwenye klabu moja ya usiku ya watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE