June 11, 2017

Baada ya Aishi Manula kusaini mkataba wa miaka miwili kujiunga na Simba, klabu ya Azam imemnasa golikipa wa Mbao FC Benedict Haule na kumsainisha mkataba wa miaka miwili ili kuziba nafasi iliyoachwa na Manula.
Haule amepata umaarufu baada ya kusimamishwa kwa aliyekua golikipa namba moja wa Mbao Musa Ngwegwe. Haule alifanya vizuri kwenye mechi alizosimama golini kuelekea mwisho mwa msimu na kuisaidia timu yake kukwepa kushuka daraja huku akiifikisha fainali ya Azam Sports Federation Cup.
Mechi kati ya Mbao dhidi ya vigogo vya soka nchini (Simba na Yanga) zilimpa jina baada ya kuonesha kiwango cha juu. Licha ya kupoteza mchezo kwa mabao 3-2 mbele ya Simba, kipa huyo alikuwa kwenye kiwango bora.
Alionesha uwezo mkubwa kwenye mchezo wa mwisho wa ligi dhidi ya Yanga na kuiongoza Mbao kushinda kwa goli 1-0 ushindi ambao uliwahakikishia kubaki kwenye ligi kuu kwa ajili ha msimu ujao.
Simba watamkumbuka Haule kwa kile alichokifanya kwenye uwanja wa Jamhuri Dodoma siku ya mechi ya fainali ya Azam Sports Federation Cup ambapo Simba ilishinda kwa magoli 2-1 na kuchukua taji hilo lililowapa fursa ya kucheza michuano ya Caf Confederation Cup msimu ujao.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE