June 11, 2017

Hatimaye General Manager wa MGODI wa ACACIA BULYANHULU Bw Graham ameacha kazi katika mgodi huo na kukimbia nchi. Hili limetokea masaa machache baada ya kutangazwa kuwa kamati ya Rais ya wachumi na wanasheria inatarajia kukabidhi ripoti yao kuhusu uchunguzi wa mchanga wa dhahabu (Makinikia) mapema Jumatatu ijayo jizi limeona libwage manyanga.

My Take: Kumbe ndiyo maana mtetezi wa wezi wa madini TUNDU alikuwa akiwapigia wezi hao na kuwaomba taarifa ili aweze kuwatetea. Ninatamani Sokoine angekuwa hai leo TUNDU ungeelewa maana ya uzalendo kwa vitendo.

Wakati huohuo Waziri mkuu Kassim Majaliwa amemsimamisha Kazi mkurugenzi wa uthibiti wa huduma za nishati na maji (EWURA) Bw Felix Ngamlagos.

"Kazi hii nilipewa na Mungu sikupewa na mtu yeyote, nipo tayari kutoa sadaka mwili wangu kwa ajili ya watanzania wanyonge"-----Rais John Pombe Magufuli.

Mungu mlinde Rais John Pombe Magufuli huyu ni mzalendo halisi.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE