June 11, 2017

 
 Mtu mmoja (75) amefariki katika ajali ya moto huku wengine wawili wakiwa wamejeruhiwa vibaya (wote wa familia moja) huko Lumumba Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza siku ya Ijumaa, ambapo mpaka sasa chanzo cha moto huo bado hakijajulikana.
Tukio hilo limetokea ya majira 12:30 jioni mtaa wa Lumumba ambapo inadaiwa kwamba kabla ya ajali hiyo kutokea marehemu alikua ndani ya nyumba yake pamoja na watoto wake, ndipo ghafla ulizuka moto mkali uliokuwa unaunguza nyumba yake, na kwamba kutokana na taharuki marehemu alianza kukusanya mali zake ndani ili aweze kutoka nazo nje ndipo kwa bahati mbaya moto ulimzidia na yeye kushindwa kutoka nje na kupelekea kuungua zaidi na baadae kufariki dunia.
Hata hivyo inasemekana kwamba kutokana na miundombinu mibovu ndiyo iliyopelekea kukosa haraka msaada wa zimamoto  ambapo ukuta uliopo jirani na maeneo hayo ulipelekea gari la wanajeshi wa zimamoto pamoja na jeshi la polisi kufika eneo la tukio kwa kuchelewa na kushindwa kuokoa maisha ya mfanyabiashara Maduhu Masunga, ingawa waliweza kudhibiti moto usiharibu maeneo mengine ya jirani.
Kamanda wa polisi mkoa wa mwanza  Ahmed Msangi anatoa pole kwa wanafamilia wa marehemu, ndugu, jamaa na marafiki kwa msiba akini pia anawaombea majeruhi wapone haraka na kuwataka wanafamilia waendele kuwa wavumilivu katika kipindi hiki ambapo mwili wa marehemu bado unafanyiwa uchunguzi, na kuwaasa wananchi kujitahidi kuweka vizuri miundombinu ya umeme.
Aidha thamani ya mali na vitu vilivyoteketea katika ajali hiyo ya moto bado haijafahamika, jeshi la polisi pamoja na jeshi la zima moto kwa kushirikiana na tanesco wanaendelea kufanya uchunguzi na upelelezi kuhusiana na tukio hilo ili kujua chanzo cha moto huo, majeruhi Ngalula Maduhu 39, Brian Maduhu 26, wamepelekwa hospitali ya mkoa ya Sekou Toure kwa ajili ya matibabu na hali zao zinaendelea vizuri

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE