Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
atapokea taarifa ya kamati ya pili ya wachumi na wanasheria iliyofanya
uchunguzi madini yaliyo kwenye makontena yenye mchanga wa madini
yaliyopo katika maeneo mbalimbali hapa nchini Jumatatu tarehe 12 Juni,
2017 Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Tukio hili litarushwa hewani moja kwa moja (Mubashara) kupitia vyombo mbalimbali vya habari vya redio, televisheni, mitandao ya kijamii na tovuti rasmi ya Ikulu ambayo ni www.ikulu.go.tz kuanzia saa 3:30 Asubuhi.
Wananchi wote mnakaribishwa kufuatilia matangazo hayo kupitia vyombo
vya mbalimbali vya habari ama simu zenu za mikononi kwa kutembelea
tovuti rasmi ya Ikulu iliyotajwa hapo juu.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
10 Juni, 2017
0 MAONI YAKO:
Post a Comment