July 30, 2017

 
BENKI ya CRDB imefungua rasmi tawi jipya katika Mji wa Chake chake kisiwani Pemba, Julai 29, 2017, ikiwa ni muendelezo wa utaratibu wa Benki hiyo wa kuwafikishia wananchi huduma za kibenki karibu na maeneo.  
 
Akizungumza baada ya kufungua tawi hilo,mgeni Rasmi katika Hafla hiyo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohanmed Shein alisema anaipongeza Benki hiyo kwa kuona umuhimu wa kuweka tawi lake Pemba, kwani itawafanya wananchi wa eneo hilo kujitokeza kwa wingi kuweka fedha zao. Hivyo anaimani uwepo wa tawi hilo, utawanufaisha wananchi wa Pemba.
 
Mkugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dkt. Charles Kimei akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Chakechake, Salama Salama Mbarouk wakati wa mapokezi ya Mgeni rasmi katika ufunguzi rasmi wa Tawi jipya la Benki ya CRDB lililopo katika Mji wa Chake chake, kisiwani Pemba, Julai 29, 2017.Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Ally Hussein Laay.
 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohanmed Shein akifunua kitambaa kuashiria ufunguzi rasmi wa Tawi jipya la Benki ya CRDB lililopo katika Mji wa Chake chake, kisiwani Pemba, Julai 29, 2017. 
 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohanmed Shein (katikati) akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa Tawi jipya la Benki ya CRDB lililopo katika Mji wa Chake chake, kisiwani Pemba, Julai 29, 2017. Wengine pichani kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Mwanajuma Majid Abdalla, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Ally Hussein Laay, Waziri wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira ambaye pia ni Kaimu Waziri wa Fedha na Mipando wa Zanzibar, Salama Aboud Talib na kulia ni Mkugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dkt. Charles Kimei.
 























Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohanmed Shein (katikati) akihutubia katika hafya ya ufunguzi rasmi wa Tawi jipya la Benki ya CRDB lililopo katika Mji wa Chake chake, kisiwani Pemba, Julai 29, 2017. Kulia ni Waziri wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira ambaye pia ni Kaimu Waziri wa Fedha na Mipando wa Zanzibar, Salama Aboud Talib, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Ally Hussein Laay (wa pili kushoto) pamoja na Mkugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dkt. Charles Kimei.
 















0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE