
Rais wa Chama cha wanasheria Tanganyika na Mwanasheria wa CHADEMA Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu amekamatwa na polisi Uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere, Dar es Salaam leo wakati akielekea nchini Rwanda kwenye kikao cha halmashauri ya EALS kinachotarajiwa kuanza kesho.Mbunge Tundu Lissu.
Tundu Lissu jana akiwa Dodoma aligoma kutoka katika chumba cha mahakama akidai kuwa alikuwa na taarifa za jeshi la polisi kutaka kumkamata baada ya siku kadhaa zilizopita kutoa maoni yake juu ya serikali ya awamu ya tano na Rais. Hata hivyo kiongozi huyo jana aliweza kuondoka Dodoma baada ya kuthibitishiwa kuwa polisi Dodoma walikuwa hawana mpango wowote wa kutaka kumkamata.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment