July 20, 2017

Image may contain: one or more people, people sitting and indoor


YANGA SC imemsajili kiungo chipukizi, Baruan Yahya Akilimali aliyekuwa anasoma nchini Uganda kwa mkataba wa miaka miwili.
Winga huyo wa kulia anayeweza kucheza na upande wa kushoto pia, amesaini leo mkataba wa miaka miwili kujiunga na wana Jangwani hao.
Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa amesema kwamba wamekuwa wakimfuatilia kwa muda mrefu mchezaji huyo kabla ya kuridhishwa naye na kuamua kumsajili. Baada ya kuonyesha kipaji kikubwa katika mashindano ya shule za sekondari Uganda mwaka juzi, mdogo huyo wa winga wa zamani wa Simba, Akilimali Yahya alishawishiwa kuchukua uraia wa nchi hiyo ili achezee timu ya vijana ya taifa hilo, The Kobs, lakini akakataa.
Yanga wanaamini huyo ndiye mrithi haswa wa winga wao machachari, Simon Happygod Msuva aliye mbioni kujiunga na timu ya Ligi Kuu nchini Morocco, Difaa Hassani El-Jadida, ambayo inamchukua yeye na Mtanzania mwingine, winga pia Ramadhani Singano ‘Messi’ kutoka Azam FC.
Timu hiyo yenye maskani yake mji wa El Jadida ikiwa inatumia Uwanja wa El Abdi inataka kujaribu kutwaa taji la Ligi Kuu ya Morocco, inayojulikana kama Botola, moja ya Ligi bora kabisa barani Afrika.
 
"Baada ya kumfuatilia kwa muda mrefu,benchi la ufundi la Yanga limeridhia kusajiliwa kwa chipukizi BARUAN YAHYA kwa mkataba wa miaka miwili.
.
Baruan aliyemaliza masomo ya kidato cha sita mwaka jana nchini Uganda, amekubali kusaini kandarasi hiyo na kuipa kisogo ofa ya kupewa uraia wa Uganda ili acheze kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya nchi hiyo.
Baruan ni mdogo wake na nyota wa zamani wa soka nchini Yahya Akilimali."
amesema Mkwasa
 

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE