
Club ya soka ya Dar Es Salam na mabingwa wa ligi kuu ncini kwa mara ya tatu mfululiza timu ya Yanga, imeanza rasmi maandalizi yake ya msimu ujao wa Ligi na mashindano ya kimataifa.Mabingwa hao leo wameonekana wakifanya mazoezi katika uwanja wa Uhuru jijini Dar Es salam

Lakini pia katika ripoti yake kwa wana habri, inasema hivi hapa chini
"Kikosi cha Yanga SC kimeanza rasmi maandalizi kwaajili ya msimu ujao wa ligi kuu Tanzania bara pamoja na mashindano mengine yote itakayoshiriki.
Mazoezi yanafanyika kwenye uwanja wa Uhuru kwa muda tofauti tofauti kutokana na ratiba ya mwalimu.
Ombi kwa wana habari wote ni kwamba uongozi kwa kushirikiana na benchi la ufundi wanaomba sana wanahabari kutumia dk 15 za kwanza za mazoezi kwaajili ya kupata habari zao zote wanazozihitaji kwani mara baada ya dk 15 za kwanza kumalizika hapatakuwa na ruhusa tena kwa mwana habari yeyote kufanya lolote ikiwa ni pamoja na kupiga picha au kurekodi video za mazoezi."
0 MAONI YAKO:
Post a Comment