August 03, 2017


Msanii wa muziki Dogo Janja (kushoto) na Irene Uwoya (kulia)
Msanii wa muziki wa bongo fleva, Dogo Janja kwa mara ya kwanza amefunguka kuhusu mahusiano yake, na kutoa sintofahamu kuhusu kutoka kimapenzi na muigizaji wa filamu za kibongo Irene Uwoya. 
Akizungumza na mtandao wa East Africa Television, Dogo Janja ambaye mara nyingi hapendi kuzungumzia maisha yake binafsi, ameamua kusema kuwa msanii huyo anafaa.
"Irene ni mwanamke mzuri, anavutia, kila mwanaume anayejua mwanamke mzuri anafaa kuwa naye, ila kwa upande wangu mimi namkubali sana Irene Uwoya, kwani anaigiza vizuri, hivyo namkubali kwa kazi zake pia", alisema Dogo Janja.
Hivi karibuni kumekuwa na tuhuma za Irene Uwoya kuwa na mahusiano ya kimapenzi na msanii Dogo Janja, ambapo watu wengi wamekuwa na mtazamo tofauti wakisema si sahihi kwani Irene Uwoya kwa kuwa ni ni mkubwa sana kwa Dogo Janja. Jambo ambalo Dogo Janja anaonekana kutoliafiki. 

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE