August 06, 2017

Video for CUF wahoji uhalali wa Msajili wa Vyama vya Siasa kumtambua Prof. Lipumba


THE CIVIC UNITED FRONT
(CUF – Chama Cha Wananchi)

THE DIRECTORATE OF INFORMATION, PUBLICITY AND PUBLIC RELATION
P.O.BOX 10979 DAR ES SALAAM .


MAELEZO YA UFAFANUZI WA MASUALA MBALIMBALI YANAYOENDELEA NDANI YA CUF KWA WAANDISHI WA HABARI YALIYOTOLEWA janas TAREHE 5 AGOSTI, 2017 KATIKA UKUMBI WA OFISI YA WABUNGE WA CUF-MAGOMENI, DAR ES SALAAM:

1. UTANGULIZI:
Ndugu Waandishi wa Habari,
Awali hatuna budi kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujaalia uhai na
afya njema kuweza kukutana. Tuwashukuru kwa kazi kubwa mnayoendelea
nayo ya kuuhabarisha umma wa watanzania ndani na nje ya mipaka ya
Tanzania juu ya masuala mbalimbali yanayoendelea nchini hususani ndani
ya Chama chetu cha CUF.
Kama tunavyofahamu kuwa Jana yamefanyika mazishi ya aliyekuwa Rais
(Mwenyekiti wa Taifa) wa Chama TADEA ndugu John Lifa CHIPAKA. Kwa
niaba ya Chama Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Taifa Mheshimiwa
Julius MTATIRO ambaye yupo nchini Marekani kwa masomo ya Utawala
katika Chuo kikuu nchini humo ametuma salaamu za Rambirambi kwa Chama
cha TADEA, ndugu, jamaa na marafiki na wote walioguswa na msiba huu
kwa namna moja au nyingine. “CUF imepokea kwa masikitiko makubwa
taarifa ya kifo cha John Chipaka ambaye amekuwa ni mpambanaji wa
kudai demokrasia na ni muasisi wa mageuzi nchini kabla na baada ya
Uhuru wa Tanganyika. Aliamini ktk utawala wa kidemokrasia kwa mfumo wa
uwepo wa vyama vingi nchini, jambo lilompelekea kuonekana ni mtu mbaya
kwa watawala na kuwekwa kizuizini kwa kosa la uhaini kwa miaka zaidi
ya kumi na mbili chini ya utawala wa awamu ya kwanza ya Mwalimu Julius
Nyerere. Pamoja na misukosuko aliyopitia kipindi chote hicho hakuwahi
kurudi nyuma na kubadilisha msimamo wake wa kudai uhuru wa fikra na
hoja mbadala kwa maslahi ya Taifa. Mwaka 1992 John Chipaka pamoja na
umri wake kuwa mkubwa naye alishiriki kuasisi tena mageuzi nchini kwa
kuanzisha moja ya chama cha siasa kinachojulikana kwa jina la TADEA na
yeye kuwa Rais wa chama hicho mpaka alipofariki. Hakika marehemu
Chipaka katika msimamo huo ameacha funzo kubwa kwa vijana na wazee
wenzake kuwa na moyo wa mageuzi, na ujasiri wa kupambana kudai haki na
uhuru”. Ameeleza Mheshimiwa Mtatiro. Mwenyezi Mungu amsamehe
mapungufu yake na amuweke mahala pema peponi. Amiin!!

2. KUHUSU KESI/MASHAURI YA CUF YALIYOPO MAHAKAMANI:
Kama tunavyofahamu mwaka jana mwezi wa Septemba 24, 2016 baada ya
Lipumba kufanya uvamizi wa ofisi za chama pale Buguruni kinyume na
sheria na taratibu baada ya Kujiuzulu kwa hiari yake na kuiacha ofisi
hiyo takribani kwa kipindi cha mwaka mzima. Chama cha CUF kupitia
maamuzi ya kikao cha Baraza Kuu la Uongozi la Taifa iliagiza Kamati ya
Utendaji ya Taifa kusimamia suala hilo kwa kulifikisha mbele ya vyombo
vya sheria-Mahakama ili kulipatia ufumbuzi. Ni kwa msingi huo
kuliendelea kujitokeza kwa ukiukwaji wa mambo mbalimbali na athari za
uvamizi huo na mpaka sasa kuna Mashauri 6 ya Msingi yaliyopo
Mahakamani Pamoja na mashauri madogo mengine ambayo sijayataja katika
orodha hii kama ifuatavyo;

a) Kuna shauri la msingi (Civil Application/Cause) namba 23/2016 hili
linahusu kuhoji uhalali wa maamuzi ya Msajiri wa Vyama vya siasa
nchini Jaji Franscis Mutungi kumrejesha Lipumba katika Uenyekiti
kinyume na Katiba ya CUF na maamuzi ya Mkutano Mkuu wa Taifa. Lipo
mbele ya Jaji Kihiyo na limepangwa kutajwa Tarehe 7/9/2017.
b) Kuna shauri la msingi la madai (Civil Application no. 21/2017)
kuhusu wizi wa Ruzuku na shauri dogo (Miscellaneous Civil Application
No.28/2017) hili linahusu kuhusu kuweka Zuio [Injuction] kutolewa
Ruzuku ya Chama kutokana na wizi wa shilingi 369 zilizoibwa na Lipumba
na kundi lake wakishirikiana na Msajili Jaji FRANCIS Mutungi.
Limepangwa kutolewa maamuzi ya Pingamizi Tarehe 11 Agosti, 2017 Lipo
Mbele ya Mheshimiwa Jaji Wilfred Ndyansobera.
c) Kuna Shauri La Madai Namba 13/2017 Lililofunguliwa Na Ally Salehe
dhidi ya RITA, Lipumba na wenzake kuhusu uhalali wa Bodi FEKI ya
Wadhamini ya CUF iliyosajiliwa na RITA. Na shauri dogo namba 51/2017
linaloomba kuwepo kwa zuio (Injuction) ya kuizuia bodi hiyo kufanya
kazi mpaka shauri la msingi litakaposikilizwa na kufanyiwa maamuzi.
Limepangwa kutajwa na au kusikilizwa tarehe 11 Agosti, 2017. Nalo lipo
mbele ya Mheshimiwa Jaji Ndyansobera.
d) Kuna shauri la Jinai namba 50/2017 kuhusu Lipumba na wenzake, Emmy
Hudson -RITA, Jaji FRANCIS Mutungi kughushi nyaraka na kutaka
kuingilia mwenendo wa mashauri yaliyopo Mahakama (CONTEMPT OF COURT
PROCEEDINGS)
e) Kuna shauri la msingi (Election Petition) namba 1/2017
linalohusiana na uchaguzi wa wajumbe wa Bunge la Afrika Mashariki
katika Mahakama kuu ya Dodoma kati ya Twaha Taslima, Abdallah Mtolea,
Katani Ahmed katani dhidi ya Bunge kwa kukiuka utaratibu na kanuni za
uchaguzi huo uliompa Mohamed Habibu Mnyaa uwakilishi wa CUF hali si
mwanachama.
f) SHAURI LA MSINGI (CIVIL CASE NO.143/2017) Juu ya Wabunge 8 wa CUF
na Madiwani 2 kupinga kuvuliwa uanachama na Lipumba lakini pia kuna
maombi madogo (Miscelleneous Civil Application No. 447/2017) ambayo
inahusiana na kuomba Zuio la muda (Temporary Injuction Order and To
maintain Status Quo)

UFAFANUZI WA KILICHOTOKEA NA MAAMUZI YA MAHAKAMA KUU:
Shauri la msingi (CIVIL CASE NO. 143/2017) Limepangwa
kusikilizwa/kutajwa Tarehe 31/8/2017 shauri hili lililofunguliwa na
wabunge wetu 8 na Maadiwani wawili wa manispaa za ubungo na Temeke
ambao ni

1. MIZA BAKARI HAJI
2. SAVERINA SILVANUS MWIJAGE [MBUNGE]
3. SALMA MOHAMED MWASA [MBUNGE]
4. RAISA ABDALLAH MUSSA [MBUNGE]
5. RIZIKI SHAHRI NG’WARI [MBUNGE]
6. HADIJA SALUM ALLY AL QASSIM [MBUNGE]
7. HALIMA ALI MOHAMED [MBUNGE]
8. SAUMU HERI SAKALA [MBUNGE]
9. ELIZABETH ALATANGA MAGWAJA- DIWANI VITI MAALUMU MANISPAA YA TEMEKE.
10. LAYLA HUSSEIN MADIBI- DIWANI VITI MAALUM-MANISPAA YA
UBUNGO.

DHIDI YA
1) BODI YA WADHAMINI -CUF,
2) MWENYEKITI WA CHAMA TAIFA,
3) KAIMU KATIBU MKUU-CUF,
4) MKURUGENZI TUME-NEC,
5) KATIBU WA BUNGE,
6) MKURUGENZI MANISPAA- TEMEKE
7) MKURUGENZI MANISPAA -UBUNGO
8) RUKIA AHMED KASSIM,
9) SHAMALA AZIZ MTAMBA,
10) KIZA HUSSEIN MAYEYE,
11) ZAINAB MNDOLWA AMIR,
12) HINDU HAMIS MWENDA,
13) SONIA JUMAA MAGOGO,
14) ALFREDINA APOLINARY KAHIGI,
15) NURU AWADH BAFADHILI

Wabunge na Madiwani Wetu wanadai haki ya uanachama wao kwa kuhoji
mchakato uliotumika kufikia maamuzi hayo ambao haukufuata katiba ya
CUF na huku kukiwa na mashauri ya msingi yanayoendelea mahakamani
yanayohoji uhalali wa Uongozi juu ya ‘Mgogoro uliopandikizwa na Vyombo
vya dola kwa kumtumia Msajili wa Vyama vya siasa unaoendelea. Wanahoji
juu ya uhalali wa vyombo vilivyochukua hatua hizo za nidhamu dhidi yao
kama zimefuata taratibu ikiwa ni pamoja na kuwapatia taarifa za tuhuma
zao kwa maandishi ili waweze kujiandaa kwa utetezi, siku na tarehe ya
kikao hicho ukizingatia kuwa si wote wanaoishi hapa Dar es Salaam,
uharaka wa Bunge na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuchukua hatua bila
kujiridhisha na alau kiubinaadamu Bunge ikiwa ni wajumbe wake
kuwauliza na kujua kutoka kwako hicho kilichojitokeza, kwa ujumla
hawakupewa nafasi ya kusikilizwa na kujitetea, maamuzi hayakuzingatia
haki za kikatiba ikiwemo kukata Rufaa ndani ya siku 14 Ibara ya 108(5)
ya katiba ya CUF, Wabunge wamekatia Rufaa maamuzi hayo na kumuandikia
barua na kukiomba Chama kupitia Katibu Mkuu kiweze kuitisha Mkutano
Mkuu wa Taifa ili kufikisha rufaa yao. Mkutano Mkuu ndio wenye mamlaka
na maamuzi ya mwisho juu ya masuala yote ndani ya Chama. Hilo
lilifanywa na Lipumba na wenzake pale Baraza Kuu la uongozi taifa
lilipowachukulia hatua za kinidhamu kwa kuwasimamisha uanachama Tarehe
28 Agosti, 2017.
Hayana mengine ndiyo yanayohojiwa Mahakamani katika shauri hili la msingi.

3. KUHUSU SHAURI DOGO LA MADAI [MISCELLENEOUS CIVIL CASE NO. 447/2017]
WABUNGE [8] NA MADIWANI [2] WA CUF DHIDI YA walalamikiwa walewale 15
tajwa hapo juu.

Maombi hayo yanahusu kuiomba Mahakama Kuu itoe zuio la muda [Temporary
Injuction Order and to maintain Status Quo- HII MAANA YAKE NI
KUSIMAMISHA MAAMUZI YA BUNGE NA TUME NA KUWAREJESHA WABUNGE WALIODAIWA
KUVULIWA UANACHAMA WAENDELEE NA SHUGHULI ZA BUNGE NA KUWAWAKILISHI
HALALI] katika kipindi hiki mpaka hapo shauri la msingi
litakapoamuriwa. Kabla maombi hayo hayajasikilizwa Walalamikiwa
(Respondent's No.1,2,3,4,5,8-15) waliweka Pingamizi la Awali (
Preliminary Objections) juu ya shauri hilo kwa madai ya kukosa sifa za
kisheria (incompetence enacted provisions of law) na hoja hizo 4 za
pingamizi zilizosikilizwa takribani kwa masaa 4 Tarehe hiyo 2/8/2017
pale shauri hilo lilipoitwa kwa kusikilizwa na baadae kupangwa
kutolewa maamuzi ya Pingamizi hilo jana Tarehe 4/8/2017.

4. MAAMUZI JUU YA PINAMIZI LA AWALI YALIYOTOLEWA NA MAHAKAMA KUU;
Katika kupitia hoja zilizowasiilishwa Mahakamani hapo katika pingamizi
hilo la awali (Preliminary Objection) lililowekwa na walalamikiwa
Mahakama Kuu imekubaliana na hoja za waweka pingamizi kuwa kifungu cha
sheria kilichotumika kufungulia shauri hilo mahakamani sio sahihi na
hivyo kuliondoa shauri hilo kwa maana ya ‘STRUCK OUT”

Unapozungumzia pingamizi unazungumzia hoja za kisheria pekee (pure
points of law) kati ya hoja 4 zilizowasilishwa hoja 3 zimekataliwa na
moja kukubaliwa iliyohusiana na matumizi ya sheria za uingereza
(Common Law) section 2(3) ya JALA kifungu ambacho kwa mtazamo/maoni
ya Jaji hakiipi mamlaka ya kisheria Mahakama kusikiliza maombi hayo.
Nini maana ya maamuzi hayo na tafsiri ya kisheria juu ya neno “Struck
out na Dismissal”

LEGAL DEFINITION :
"Difference between DISMISSAL and STRIKE OUT. When a case is
dismissed, there is no right to reinstate it in the future. This is
the legal way to say the case is closed and it cannot be re-opened.
When a case is struck out, it may be re-opened.

TAFSIRI YA KISHERIA:
“Tofauti kati ya kufuta na kuondoa (shauri) ni kwamba kesi ikifutwa,
hakutakuwa na haki ya kuirejesha tena (kurudisha/kuifungua upya) hapo
baadae. Hii ni njia ya kisheria kusema kuwa kesi imefikia mwisho na
huwezi kuifungua upya. Pale kesi inapoondoshwa, inaweza kufunguliwa
upya.”

Pingamizi juu ya maombi ya Shauri namba 447/2017 yameondolewa mbele ya
Mahakama na wala hakuna hiko kitu kinachoitwa ‘kesi imefutwa, au
kutupiliwa mbali au mahakama imeruhusu Wabunge wapya kuapishwa, KWA
HAKIKA HAKUNA USHINDI WA MAAMUZI YALIYOTOLEWA’ kama inavyoripotiwa.
Shauri limeondolewa kwa kumaanisha kama vile hakukuwa na kitu
kilichopaswa kujadiliwa na Mahakama juu ya maombi hayo. Pingamizi la
awali [Preliminary Objection] na Maombi ya Zuio [injuction/Stop Order]
ni vitu viwili tofauti kisheria. Wabunge wa CUF wameomba Zuio. Lipumba
na wenzake wameweka Pingamizi. Huo ndio usahihi wa maelezo ya nini
kilichojitokeza katika maamuzi ya Mahakama Kuu jana.

5. MATOKEO YA MAAMUZI YA MAHAKAMA KUU;
Maamuzi hayo yametupa fursa ya kuandaa vizuri zaidi nyaraka hizo na
tayari tumepata faida ya kujua hoja wanazosimamia walalamikiwa
(Respondents). Wabunge wetu wameweza ndani ya masaa 2 baada ya maamuzi
tayari nyaraka zilitayarishwa, kusainiwa pamoja na marekebisho yote ya
msingi na ya lazima yaliyopaswa kuingizwa ikiwemo kuwajumuisha katika
shauri hilo Wakurugenzi wa Manispaa za Ubungo na Temeke ambao
wanahusika kutokana na Madiwani waliopo katika halmashauri zao
kuathiriwa na maamuzi ya Lipumba na genge lake. Ni matarajio yetu kuwa
Jumatatu ya tarehe 7/8/2017 tutapata mrejesho wa kujua Mahakama Kuu
imelipanga lini kulisikiza shauri hilo kutokana na kuingizwa kwa hati
ya dharura/haraka (Under Certificate of Urgency).

6. WITO KWA WAAANDISHI WA HABARI, WANACHAMA NA WATANZANIA KWA UJUMLA:
KESI ni MCHAKATO siyo TUKIO. Utaratibu wa kisheria una njia na namna
kadhaa za kupitia ili kuifikia haki inayopiganiwa. Tunawaomba
waandishi wa habari kuripoti habari za kimahakama kwa uashihi na
kutumia weledi ili kuepusha taharuki na kuwachanganya wananchi na
wadau mbalimbali wa habari. Tusitoe taarifa kwa kutumia ‘mizuka’
mkanganyiko uliojitokeza jana na leo katika vyombo vya habari
haukujenga weledi na afya njema kwa kuwahabarisha wananchi ndivyo
sivyo.

Tunatoa wito kwa wanachama wa CUF, Wapenzi na Watanzania kwa ujumla
kupuuza habari za upotoshaji na propaganda zinazoendelea kufanyika
kupitia mitandao ya kijamii na vyombo mbalimbali vya habari. Si shauri
la msingi wala maombi ya zuio lililosikilizwa na Mahakama Kuu na
kuyatolea maamuzi. Kilichotolewa maamuzi ni Pingamizi juu ya hoja za
za kisheria pekee ambazo zimesharekebishwa na kurejesha upya shauri
hilo mahakamani.

Tuendelee kuwa watulivu na kwamba viongozi wenu ngazi ya Taifa wapo
makini kulisimamia suala hili na kuhakikisha kuwa haki inapatikana.
Tuna imani kubwa na Mahakama kuwa ni chombo cha kusimamia haki si
Chombo cha kuchezewa. Maamuzi ya Mahakama Kuu juu ya pingamizi
tumeyapokea, ni sahihi kwa mujibu maoni ya Jaji kwa mujibu wa sheria
na wala SI HUJUMA DHIDI YA HAKI kama inavyotaka kuaminishwa na baadhi
ya wasiojua taratibu na misingi ya kisheria. Hakuna maamuzi yoyote
mpaka sasa yaliyotolewa na Mahakama Kuu katika kadhia hii inayoendelea
zaidi ya Kuzuia Ruzuku isitolewe kwa Lipumba na genge lake na hili la
kuondoa maombi madogo yaliyowasilishwa.

Tutaendelea kukilinda na kukitetea Chama chetu cha CUF kwa nguvu zetu
zote na kukiimarisha zaidi ilii kiendelee kutekeleza wajibu wake
katika uendeshaji wa siasa za kistaarabu, na kwa njia za amani na
zinazofuata Katiba ya CUF, Katiba ya JAMHURI ya Muungano wa Tanzania
na Sheria nyingine za nchi yetu.

CUF NI TAASISI IMARA, YENYE VIONGOZI MAKINI.
HAKI SAWA KWA WOTE
MBARALA MAHARAGANDE
K/ NAIBU MKURUGENZI WA HABARI, UENEZI, NA MAHUSIANO NA UMMA-CUF TAIFA.

0715 06577/ 0767 062577
maharagande@gmail.com

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE