
Kocha wa Bayern Munich Carlo Ancelotti amefutwa kazi leo kufuatia mwanzo
mgumu wa msimu wa 2017/18 yakiwemo matokeo ya jana usiku ambapo timu
hiyo ilikubali kichapo cha mabao 3-0 kutoka kwa PSG.
Mkurugenzi
mtendaji wa Bayern Munich Karl-Heinz Rumminigge alionekana kuchukizwa
na matokeo ambapo alisema Bodi ya timu itakuwa na kikao na kocha
Ancelotti mchana wa leo baada ya timu kurejea kutoka Paris Ufaransa.
Mchana wa leo Sky Sports imethibitisha kuwa
baada ya kikao Bodi imefikia maamuzi ya kusitisha kibarua cha kocha
huyo raia wa Italia.
Ancelotti mwenye miaka 58 ameitumikia
Bayern kwa msimu mmoja wa 2016/17 baada ya kuchukua nafasi ya Pep
Gaurdiola ambaye alijiunga na Manchester City. Muitaliano huyo
ameiwezesha Bayern kutwaa ubingwa wa Bundesliga msimu uliopita.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment