
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe
amefunguka na kusema kuwa endapo watashindwa kufanya maandalizi mazuri
ya michuano ya mataifa ya Africa (AFCON) kwa vijana 2019 basi Watanzania
hawawezi kumuelewa.
Mwakyembe
amesema kuwa Tanzania ndiyo iliomba kuwa mgeni wa michuano hiyo mwakani
hivyo wanapaswa kufanya maandalizi ya kutosha ili waweze kufanya vizuri
katika michuano hiyo na kusema kama hawatafanya maandalizi mazuri basi
watachekesha.
"Ndugu zangu hatuna sababu
kabisaa za kutojiandaa vizuri tutachekesha na hamtatusamehe Watanzania
tukishindwa kujiandaa vizuri, nashukuru sana kwamba na timu nzuri sana
na tulianza muda mara tu baada ya uchaguzi yapo mambo mengi sana kuhusu
suala hili lakini uzuri ni kwamba tumeanza kuyangalia kuhusu viwanja vya
mazoezi, masuala ya usafiri, usalama hata maandalizi ya timu yetu
yenyewe nayo ni mchakato mkubwa" alisema Mwakyembe
Aidha Mwakyembe amesema kuwa katika kipindi kilichobaki anaamini kuwa watafanya maandalizi makubwa sana
0 MAONI YAKO:
Post a Comment