
Wasanii wakongwe kwenye game ya muziki ambao ni ndugu wa familia moja
Unique Sisters, wamesema wamerudi rasmi kwenye game, kutokana na maombi
ya mashabiki na kuachia kazi yao mpya kwa ajili yao inayoitwa 'Kwako
wewe'.
Wakizungumza na mwandishi wa East Africa Television, mmoja wa wasanii
wanaounda kundi hilo Rahima ambaye ndiye mkubwa wao, amesema walikuwa
kimya kutokana na majukumu ya kifamilia, ambapo wawili miongoni mwao
wameshaolewa, lakini wameona kiu ya mashabiki imekuwa kubwa.
“Tulikuwa tunapata maoni kutoka kwa mashabiki tuko kimya sana
tukasema tunataka kurudi, tulikuwepo na tumerudi, tumerudi kuonyesha
kipaji chetu ili kuwafurahisha mashabiki wetu, sio kushindana na mtu
yeyote”, amesema Rahima.
Akiendelea kuelezea hayo Radhina ambaye ndiye mdogo kwenye kundi hilo
amesema pia wamekuja kuleta ladha tofauti ya muziki, ili kuleta
changamoto zaidi kwenye game upande wa wanawake.
“Na pia ni vizuri kuwa na vitu tofauti, vionjo tofauti na watu
tofauti ambao wanafanya muziki, ndio maana tumerudi ili kutoa 'option'
hiyo, kuna mwengine ataimba kwa vingine, kwa hiyo tutoe 'option' kwa
mashabiki waweze kupata vitu vingi na vionjo vingi vya kusikiliza kutoka
kwa wanawake”, amesema Radhina.
Pia wasanii hao wameendelea kwa kusema kwamba wamefurahi kuona jinsi
game ilivyobadilika siku hizi na kuwa na wasanii wengi wa kike, tofauti
na kipindi cha nyuma ambapo wasanii wa kike walikuwa wachache.
“Tunafurahi kwamba wanawake tumejitokeza sasa hivi kwa sababu
nakumbuka miaka ya zamani tulikua tyunajaribu sana kuwaita wanawake,
sasa hivi watu wamesikia wamejitokeza”, amesema Rahima.
Kundi hilo mla Unique Sisters linaundwa na ndugu wa familia moja, Rahima Kipozi, Radhia Kipozi na Radhina Kipozi.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment