October 10, 2017


 

Kiongozi mkuu wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga ametangaza kujiengua kwenye kinyang’anyiro cha uchaguzi mkuu ambao umepangwa kufanyika tarehe 26 Oktoba mwaka huu.
Bwana Odinga amesema anataka kufanyike uchaguzi mpya wa haki na halali kama ilivyoamuliwa na mahakama ya juu mapema mwezi septemba.
Akitaja sababu za kujiondoa, Odinga amesema amejiondoa ili kuipa tume ya uchaguzi nchini humo (IEBC) muda wa kutosha kufanya mabadiliko ambayo yatawezesha kufanyika uchaguzi kwa njia iliyo huru.
Uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika tarehe 26 Oktoba mwaka huu, utakuwa ni marudio ya uchaguzi mkuu, baada ya mahakama ya juu nchini Kenya kufuta matokeo ya uchaguzi wa tarehe 8 mwezi Agosti mwaka huu.
Matokeo ya awali ya tume ya uchaguzi yalimtangaza Rais Uhuru Kenyatta kuwa mshindi.

Related Posts:

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE