December 13, 2017


 
 Idara ya Uhamiaji nchini imesema sakata la kumuhoji uraia wake Askofu wa Jimbo la Ngara , Severine Niwemugizi, wataweka wazi pindi uchunguzi utakapokamilika.
Hayo amesema jana  na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dr. Anna Makakala.
''Hizo ni taarifa za kiuchunguzi ambazo bado tunaendelea nazo, huwezi kuweka wazi kila kitu wakati bado tupo katika uchunguzi, tunapokuwa na shaka na mtu yoyote kuhusu uraia wake tunaruhusiwa kumuhoji,'' amesema Dr. Makakala.
Madai ya Askofu huyo kuhusu kuhoji upatikanaji wa katiba mpya ndio sababu ya kuhojiwa na idara hiyo, Dr. Anna amekanusha na kusema wawaache kwanza hadi uchunguzi utakapokamilika.
''Hayo ya kwake, naomba tusubiri uchunguzi hadi utakapo kamilika,'' ameongeza

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE