January 20, 2018


 
Muongozaji wa video nchini Tanzania, Msafiri Shabani maarufu Travela  wa kampuni ya Kwetu Studios, ameeleza mipango yake katika mwaka 2018.
Akiongea na TVE katika kipindi cha Eight, Travela amesema alikuwa na ndoto za kufanya kazi na wasanii wa nje katika mwaka huu ambapo tayari ameshapata dili kutoka kwa wasanii kumi mpaka sasa.
“Mwaka jana nilikuwa na dream kuwa mwaka huu lazima nifanye video na wasanii wa nje. Mpaka sasa kuna wasanii kama kumi wa nje ambao nataka nifanye nao,” amesema muongozaji huyo wa video.
Akiongea kuhusu watu wanavyozungumza video zake kukosa stori, Msafiri amesema hilo linatokana na tatizo kubwa la mashabiki wengi wamekuwa wakitengeneza script zao vichwani kabla ya video ya wimbo haijatoka.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE