January 18, 2018

 

UONGOZI wa Simba SC umeamua kuachana na kocha Hubert Velud na kumchukua Mfaransa mwenzake, Pierre Lechantre. Taarifa ya klabu ya Simba leo kwa vyombo vya Habari imesema kwamba, kocha huyo mzoefu ataanza kazi mara moja na atasaidiwa na kocha Mrundi, Masoud Juma ambaye amekuwa akiiongoza timu tangu Desemba mwaka jana alipoondolewa Mcameoon, Joseph Marius Omog. Taarifa hiyo imesema Lichantre amekuja na msaidizi mmoja, kocha wa viungo, Mmorocco Mohammed Aymen Hbibi na jioni ya leo ataishuhudia Simba ikicheza na Singida United kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara. Pierre Lechantre aliyezaliwa Aprili 2, mwaka 1950 mjini Lille, Nord, Ufaransa ni kocha aliyeipa Cameroon ubingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka 2000 na kabla ya kuanza kufundisha alikuwa mchezani pia. Aprili 27 mwaka 2012, Lechantre alitambulishwa kuwa kocha Mkuu wa Senegal, lakini akashindwa kufikia makubaliano ya mwisho na Shirikisho la Soka la nchi hiyo

                      

Related Posts:

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE