February 20, 2018

Viongozi mbalimbali wakiwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selemani Jafo wakikagua miundombinu iliyojengwa kwa shule ya msingi Kitongamango.

 
 
                 Madarasa mapya yaliyojengwa katika shule ya msingi Kitongamango.
 
 
 Wanafunzi wa Shule ya msingi Kitongamango wakimpokea Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selemani Jafo.
              Jengo la Ofisi ya Walimu na madarasa katika shule ya msingi Boga.
 
Majengo mapya ya Shule ya msingi Boga.

Wanafunzi wa shule za msingi Kitongamango na Boga wilayani Kisarawe  wameishukuru serikali kwa kuwajengea madarasa mapya, vyoo vya kisasa pamoja na Ofisi za walimu za walimu katika shule zao.

Shukrani hizo wamezitoa kwa serikali wakati wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selemani alipokuwa akizindua miundombinu hiyo katika shule hizo.

Shule hizo pamoja na shule ya msingi Mitengwe zilikuwa katika hali mbaya ya miundombinu hiyo lakini kwasasa zimejengewa na kuonekana za kisasa.

Miundombinu iliyojengwa ni pamoja na vyumba vya madarasa 4, vyoo matundu 10, na Ofisi za walimu kwa kila shule, hali ambayo imebadili mazingira ya shule hizo.

Kufuatia hali hiyo, Wanafunzi hao wamemshukuru Rais Dkt. John Pombe Magufuli na Mbunge wa Kisarawe Selemani Jafo  kwa kubadilisha shule zao kwa kuweka mazingira mazuri ya kusomea.

Wamemuahidi Waziri Jafo kusoma kwa bidii katika na kufanya vizuri kwenye masomo yao.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE