April 18, 2018

Image may contain: 1 person
 Mbunge wa Kigoma mjini na kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo Ndg. Zitto Zuberi Kabwe Ruyagwa, ameandika katika ukurasa wake wa Facebook kwamba yupo tayari kukamatwa  ama kuuawa kwa kusema juu ya upotevu wa Fedha zinazokadiliwa ni shilingi Trilioni 1.5 mali ya watanzania. Zitto anaandika hivi,

"Kuna mtu anasema nikamatwe kwa kupotosha Kuhusu TZS 1.5trn zinazohojiwa na CAG.
Mimi Kabwe Zuberi Ruyagwa Zitto, Mwenyeji wa Kigoma, Muislam, NAAPA kwamba Serikali ya CCM ya Awamu ya Tano imeshindwa kuonyesha kwa CAG matumizi ya shilingi trilioni MOJA na Bilioni MIA TANO.
Nipo tayari kukamatwa kwa kusema hivyo ( haitafuta ukweli wa ubadhirifu huo ). Nipo tayari kuuwawa kwa kusema hivyo ( mawazo yangu hayatakufa).
Eeh Mwenyezi Mungu nisaidie"

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE