May 18, 2018

Image may contain: 5 people, people standing and outdoor
Peter dogo anataka nafasi huyo, jiandae kumpisha...゛ni maneno ya Alphonce Modest akimtania aliyekuwa golikipa namba moja wa Taifa Stars, Peter Manyika wakati wakiwa safarini katika basi kuelekea Mwanza, Oktoba, 2001.
Modest alikuwa akimwambia maneno hayo Manyika huku akimuonyesha kijana aliyekuwa na miaka 18 wakati huo- golikipa Juma Kaseja.
Stars ilikuwa ikienda Mwanza kucheza mchezo wa fainali wa michuano ya Castle Cup vs Kenya- Harambee Stars baada ya kuwashinda DR Congo katika nusu fainali pale Sheikh Amri Abeid Stadium, Arusha.
Katika vikosi bora vya Stars katika karne hii-kile kilichoshinda ubingwa wa Castle mwaka 2001 ni bora kuliko vyote.
Manyika- golini
Mecky Mexime- beki ya kuume
Modest - beki ya kushoto
Boniphace Pawasa- beki ya Kati
John Mwansasu- beki ya kati
Waziri Mahadhi/Suleimani Matola- namba sita
Said Maulid ‘SMG‘- namba saba
Salvatory Edward- namba nane
Ntenze John- mshambulizi wa Kati
Joseph Kaniki...
Modest ni mshindi - mtu aliyesaidia mpira wa Tanzania na kutupa kikombe. Kwa sasa anapitia ‘ibada‘ na ni muda mrefu sana anaumwa-yupo Turiani, Morogoro.
Ni vyema-wachezaji, TFF, Serikali kumsaidia wakati huu.
PoleSanaModest

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE