July 08, 2018

Image result for maharagande
Chama cha wananchi CUF, Kimetangaza rasmi kujitoa katika kinyang'anyiro cha uchaguzi wa marudio unaotarajiwa kufanyika mwezi ujao nchini. Akitoa taarifa kwa umma Naibu Mkurugenzi wa Habari , Uenezi na Mahusiano ya Umma wa chama hicho Mbarala Maharagande amesema, wameamua kuitoa katika chaguzi hizo kutokana na mgogoro unaoendelea ndani ya chama chao

Chama Cha Wananchi) Kinapenda kuwajulisha wanachama wa CUF na Watanzania kwa ujumla kuwa Kamati ya Utendaji ya Taifa imefanya uchambuzi wa kina na tathmini pana juu ya taarifa ya kufanyika kwa uchaguzi mdogo wa marudio katika Kata 79 na majimbo 2. Chama cha CUF HAKITOSHIRIKI katika uchaguzi huu mdogo wa marudio uliopangwa kufanyika nchini kote Tarehe 12 August, 2018. Sababu za Msingi za Kutoshiriki katika Uchaguzi Huu ni nyingi moja wapo ikiwa ni;
Mkanganyiko wa uongozi katika usimamizi wa uchaguzi huo uliojitokeza kutokana na Mgogoro uliopandikizwa ndani ya CUF na Lipumba na washirika wake. CUF inaona ni busara kwa sasa kuelekeza nguvu na rasilimali zake chache zilizopo katika kushughulikia na kuupatia ufumbuzi Mgogoro huu uliopandikizwa.
THE CIVIC UNITED FRONT-CUF Inatoa wito kwa Vyama rafiki vyote katika UKAWA kukaa pamoja kufikia muafaka na maridhiano na kusimamisha Wagombea bora, Imara, na madhubuti kugombea nafasi hizo zote.
CUF inatoa wito kwa Viongozi na wanachama wake wote katika maeneo yote ya marejeo ya Uchaguzi kwa Tanzania Bara kushirikiana bega kwa bega na kuunganisha nguvu za pamoja na Vyama rafiki vya UKAWA katika uchaguzi huu ili KUISHINDA CCM NA VIBARAKA WAKE.
UHALISIA[REALITY]:
Katika kata 79 zilizotangazwa, CUF imepoteza Kata 5 ilizokuwa inaziongoza kwa Madiwani wake kununuliwa na CCM- Kata mbili zipo manispaa ya Jiji la Tanga Mjini na Kata moja Mtwara Vijijini na Diwani mmoja Kufariki [Wilaya ya Kwimba] na Kondoa Kutokana na vigezo vya kitaalamu na kitakwimu (Election Strategies) na Ramani ya maeneo utakapofanyika Uchaguzi huu wa marudio CUF ingeweza kushiriki kikamilifu katika Kata za Mkakati 11 pekee [5+6]. Na Kata zingine CUF ingelazimika kuunganisha Nguvu na Vyama vingine katika UKAWA.
Huu ndio Msimamo wa Chama unaozingatia maslahi mapana ya CUF (Taasisi) unaopaswa kuheshimiwa na kuzingatiwa na kila mwanaCUF wa kweli.
KUHUSU UCHAGUZI WA JIMBO LA JANG’OMBE,UNGUJA-ZANZIBAR UNAOTARAJIWA KUFANYIKA TAREHE 27/10/2018;
CUF ilishaweka wazi msimamo wake kwamba HAITASHIRIKI katika uchaguzi huo kutokana na ukweli kwamba msingi wa uchaguzi huo unatokana na uchaguzi Haramu wa Tarehe 20/3/2016 ambao ndio uliwaweka Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Haramu, Madiwani Haramu na Serikali Haramu. CUF inatoa wito kwa Wananchi wote wapenda Demokrasia ya Kweli kutoshiriki kwa namna yoyote ile katika uchaguzi huo.
TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI (NEC):
NEC imetangaza kufanyika kwa uchaguzi mdogo katika Jimbo la Buyungu, Mkoani Kigoma [Lililokuwa linaongozwa na Mbunge wa CHADEMA aliyefariki dunia hivi karibuni] na kwenye Kata 79 za Tanzania Bara.
Taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Taifa Jaji Kaijage imeeleza kuwa uchaguzi huo mdogo utafanyika ndani ya Halmashauri 43 zilizopo kwenye Mikoa 24 ya Tanzania Bara. Mikoa hiyo ni pamoja na, Kigoma, Arusha, Dar es Salaam, Dodoma, Iringa, Kagera, Katavi, Kilimanjaro, Lindi, Manyara, Mara, Mbeya, Mtwara, Morogoro, Mwanza, Njombe, Rukwa, Ruvuma, Shinyanga, Simiyu, Singida, Songwe, Tabora na Tanga.

Kwa upande wa Halmashauri zitakazokuwa na Uchaguzi ni Moshi, Ruangwa, Mbulu, Hanang, Babati, Serengeti, Tarime, Kyela, Mtwara, Newala, Kilombero, Kilosa, Kwimba, Makete, Wanging’ombe, Kalambo, Songea, Msalala, Meatu, Singida, Songwe, Tunduma, Tabora, Nzega, Urambo, Tanga, Karatu, Longido, Arusha, Ngorongoro, Monduli, Meru, Ubungo, Kondoa, Mpwapwa, Chamwino, Iringa, Kyerwa, Misenyi, Muleba, Nsimbo, Kasulu na Same.
 
HAKI SAWA KWA WOTE
Imetolewa leo Tarehe 8 July, 2018
Na. Kurugenzi ya Habari –CUF Taifa

_________________________
MBARALA MAHARAGANDE
NAIBU MKURUGENZI WA HABARI, UENEZI
NA MAHUSIANO NA UMMA

maharagande@gmail.com
MAWASILIANO: 0784 001 408/0715 062 577

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE