
Aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani bi. Happyness Seneda, amewaaga wananchi wa Kisarawe huku akiwataka waoneshe ushirikiano kwa mkuu mpya wa Wilaya hiyo bi. Jokate Mwegelo. katika ukurasa wake wa Facebook. Happyness Seneda ameandika
Ndugu zangu wana Kisarawe, wa ukae ninawashukuru sana kwa ushirikiano mlionipa tokea siku ya kwanza nakanyaga ardhi ya Kisarawe mpaka muda huu ambao Mhe. Rais imempendeza mimi kuhamia kituo kingine cha kazi na kwa nafasi nyingine!! Kwa umoja wetu tulifanya mengi na tulipanga kufanya mengi!!
Kwa kweli nitawamiss sana sana, Mungu awabariki sana endeleeni
kudumisha umoja, mshikamano na ushirikiano bila kujali dini, itikadi
wala kabila na hakika Mungu atafanya makubwa katika wilaya ya Kisarawe.
Ninaomba mumpatie ushirikiano zaidi ya huu ndugu yangu Jokate Mwengelo, kwa kufanya hivyo Kisarawe itaendelea kwa kasi kubwa.
Mungu ibariki Kisarawe
🙏
🙏
HODI IRINGA
Ninaomba mumpatie ushirikiano zaidi ya huu ndugu yangu Jokate Mwengelo, kwa kufanya hivyo Kisarawe itaendelea kwa kasi kubwa.
Mungu ibariki Kisarawe


HODI IRINGA
0 MAONI YAKO:
Post a Comment