
Hata hivyo mashtaka hayo yanayotokana na tukio la miaka 40 iliyopita. Anadaiwa alimshikashika mvulana aliyekuwa na umri wa miaka 11 wakati huo katika jiji la New York. Mtu huyo ambaye sasa ana umri wa miaka 51 amesema uhusiano wakudhalilishwa kingono uliendelea kati yake na Askofu huyo kwa muda wa miaka miwili. Lakini McCarrik amekanusha madai ya awali.
Kiongozi wa Kanisa Katoliki amechukua hatua haraka kutekeleza ahadi aliyotoa ya kutovumilia tabia ya kufichiana siri miongoni mwa makasisi. Madai ya udhalilishaji wa kingono yanawakabili makasisi wengi ikiwa pamoja na maaskofu na makadinali ikiwa pamoja na kadinali wa Australia George Pell ambaye ni mmoja wapo wa washauri wa ndani wa baba mtakatifu. Yeye pia anakabiliwa na mashtaka ya udhalilishaji wa kiongono nchini mwake.

Kasisi wa chuo kikuu cha Kanisa Katoliki Kurt Martens ametilia maanani kwamba hii ni mara ya kwanza kwa baba mtakatifu kumwamrisha mtuhumiwa kufunga sala ya kutubu. Maaskofu kadhaa wamekabiliwa na tuhuma za udhalilishaji wa kingono kwa muda wa miaka mingi, madai yaliyolitia dosari kanisa Katoliki. Lakini kanisa hilo lilitumia mbinu ya kuwahamisha tu watu hao.
Mapema mnamo mwezi huu Askofu wa Australia alishtakiwa na kuhukumiwa baada ya kuthibika kwamba alificha uchafu wa udhalilishaji wa kingono. Kasisi huyo mwandamizi alipewa adhabu ya kuwekwa mahabusi kwa muda wa miezi 12.
Mwandishi: Zainab Aziz/APE
0 MAONI YAKO:
Post a Comment