Akizungumza na waandishi wa habari jana katika madhimiso ya kilele
cha siku ya wakulima nchini ( Nane nane ) Mkoani Simiyu, Mkurugenzi
Mtendaji wa benki ya NMB, Ineke Bussemaker alisema benki yake imeamua
kusaidia kuboresha sekta ya kiliomo kutokana na umuhimu wake katika
kuchangia ukuaji wa uchumi wa nchi na pia kuboresha uchumi wa wakulima.
Alisema kuwa mafunzo hayo ambayo bado yanaendelea sehemu mbali
mbaloi nchini yanatarajiwa kuwafikia wakulima wengi zaidi kupitia vyama
vya ushirika na hivyo vitawezesha kuboresha kilimo na kuleta mabadiliko
ya kiuchumi katika ngazi ya jamii na nchi kwa ujumla.
Bi. Bussemaker alisisitiza kuwa unatakiwa ushirikiano wa wadau mbalimbali wa mendeleo ili kusaidia sekta ya kilimo kukua kwa haraka na kuleta tija kwa wakulima na nchi kwa ujumla na kuwa ikiachiwa serikali peke yake haitaweza kuleta mabadiriko hayo kwa haraka.
Bi. Bussemaker alisema kuwa mbali na mafunzo hayo benki yake imekwisha tumia zaidi ya shilingi bilioni 100 katika kuboresha sekta ya kilimo nchini kwa kutoa mikopo mbalimbali pamoja na huduma zingine za kifedha kwa wakulima nchini.
“ Ndani ya miaka michache ijayo, tunatarajia kutumia kiasi cha shilingi bilioni 500 katika sekta kuwezesha shughuli za kilimo katika mnyororo mzima wa thamani, hivyo nawaomba wakulima kutokukata tamaa na kilimo kwani benki yao ipo pamoja nao katika kuhakikisha inaleta mageuzi ya kilimo kwa manufaa na maendeleo ya wakulima na nchi kwa ujumla” alisema Bi. Bussemaker.
Bussemaker aliwataka wakulima kutumia NMB Bank katika kuleta mageuzi chanya katika kilimo na kuinua uchumi wa Tanzania kufikia uchumi wa kati kwa kuzalisha malighafi zaidi ndani ya nchi ambazo zitatumika katika viwanda vilivyopo nchini kwa kuwa mkulima akilima zaidi viwanda vinapata malighafi zaidi.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment