MSANII nguli wa vichekesho Tanzania, Amri Athuman ‘Mzee King Majuto’
amefariki dunia majira ya saa 2:00 usiku huu wa Agosti 8, 2018 katika
Hospitali ya Taifa, Muhimbili alipokuwa amelazwa akipatiwa matibabu kwa
siku kadhaa.
Mtoto wa marehemu aitwaye Abuu amethibitisha kifo cha baba yake.
Mzee Majuto alizaliwa mwaka 1948 mkoani Tanga na kusoma Shule
Msambwini, mkoani humo, alianza kuigiza 1958 akiwa na umri wa miaka 10.
Hivi karibuni Mzee Majuto alisafirishwa na kupelekwa nchini India
ambako alipatiwa matibabu na kurejea nchini ambapo alipelekwa Muhimbili
kuendelea na tiba yake.
Mzee Majuto ndiye alikuwa muigizaji wa kwanza kuandaa kazi zake
katika mikanda na kuuza akiwa na Tanzania Film Company ( TFC), alikuwa
mwigizaji mwenye mashabiki wengi kutokana maonyesho mbalimbali,
vichekesho vyake aliyoshiriki nchi mbalimbali.
“Inna Lillahi wa inna ilayhi raji’un,.Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda;
Pumzika kwa Amni Mzee Amri Athumani
0 MAONI YAKO:
Post a Comment