December 01, 2019



 
Bondia Twaha Kiduku alipokewa kishujaa Mkoani Morogor, kufuatia mapokezi aliyoandaliwa wakati akireje mkaoni hapa baada ya kumtwangwa vilivyo bondia kutoka Afrika Kusini France Thabang Ramabolu katika pambano la utangulizi la mchuano uliowakutanisha Hassan Mwakinyo kutoka Tanzania na Arnel Tinampay kutokea Philipino mpambano ambao ulimalizka kwa Hassan Mwakinyo kuibuka mbabe kwa Point.
Twaha aliwasili Morogoro mida ya saa nane mchana na kupokewa na mamia ya wakazi wa Mji wa Morogoro na kusababisha baadhi ya shughuli kusimama kwa muda. Akizungumza nasi katika mapokezi hayo, mratibu wa mapokezi hayo Jackson Jackson Charles Busanda amesema amefurahishwa na muitikio mkubwa wa wakazi wa Morogoro licha ya kuandaa tukio kwa muda mfupi. Naye kwa upande wake Bondia Twaha amewashukuru wakazi wa Morogoro kwa mapokezi yale na kusema hana cha kuwalipa zaidi ya kuwawakirisha vema katika mashindano mengine. #hongera sana Twaha Kiduku


1 comment:

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE