March 21, 2012


MSANII nguli wa muziki wa kizazi kipya bongo, Diamond, amesema kuwa anafikiria kuimba nyimbo za taarabu baada ya kukosa mpinzani kwenye bongo fleva.
Aidha alisema kuwa katika muziki wake hakuna msanii ambaye anaweza kufikia kiwango alichokuwa nacho kwani katika kuthibitisha hilo ndani ya nyimbo zake hakuna msanii yeyote aliyemshirikisha.

Aliongeza kuwa kikubwa kinachomsukuma kufanya kila aina ya muziki ni kutokana na kipaji alichokuwa nacho kwani hakuna kitu anachoweza kushindwa kutokana na uwezo aliyokuwa nao.

Msanii huyo aliongeza kuwa bado hajaamua kufanya muziki huo rasmi lakini anafikiria kama unaweza kumletea soko kama ilivyokuwa kwa bongo fleva, ambao umemfanya ajulikane duniani kote.
“Naweza kufanya kila aina ya muziki kwa sababu nina kipaji cha kuimba nyimbo aina zote hivyo endapo nikifikia muafaka naweza kufanya kitu hicho ingawa mashabiki wangu watastuka sana,” alisema.

Hata hivyo alipoulizwa kama anatshirikiana na wasanii wakongwe wa nyimbo hizo za mipasho, alisema kuwa kwanza atasimama mwenyewe lakini baada muda ataweza kuwashikisha vichwa kama Isha Mashauzi, Mzee Yusuph na wengi kibao.

Related Posts:

  • Mgombea Ubunge Lushoto afariki Dumia Nimesoma kwa masikitiko na majonzi kuhusu ajali iliyompata kaka Mohamedi Mtoi aliyekuwa akiwania Ubunge katika jimbo la Lushoto kwa tiketi ya CHADEMA na mwavuli wa UKAWA. Familia ya Mtoi … Read More
  • [picha] Tamasha la "Wasanii wa Mabadiliko" Msanii Mkoloni akiimba katika Tamasha la Wasanii wa Mabadiliko lililofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita mjini Mtwara. Lengo la Tamasha hilo ni kuwahimiza wananchi kujitokeza kupiga kura Oktoba 25, 2015. Wananchi waliojit… Read More
  • Magazetini leoLeo hii september 8 2015, tuakupa fursa ya kutazama vichwa vya habari vya magazeti ya leo hii kama yalivyotufikia … Read More
  • New Audio| Saoti Sol - Isabella |Download & Listen The award-winning Kenyan group - Sauti Sol – release ISABELLA, the sixth single off Sauti Sol’s upcoming third album: LIVE AND DIE IN AFRIKA, set for release in 2015. The acoustic ISABELLA is a bonafide ballad, and tru… Read More
  • New Audio| R.O.M.A - Viva R.O.M.A Viva| download & Listen Katika kuelekea kipindi hiki cha uchaguzi kwa Tanzania, msanii na mwana harakati R.O.M.A Mkatoliki, amekuletea wimbo huu mpya na mwenyewe akisema kama zawadi kwa watanzania wote waupate na kuuskiliza.  Download … Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE