DIAMOND AKIFANYA KWELI
MWANAMUZIKI nyota wa Tanzania wa Bongo flava, Naseeb Abdul ‘Diamond
Platnumz” juzi usiku aliweza kuuteka umati wa wageni maalum uliofurika
kwenye ukumbi wa jumba la shindano la Big Brothe stargame, na afrika kwa ujumla kwa kupiga shoo kali na ya aina yake ,nchini Afrika Kusini.
Katika shoo hiyo ambayo pia ilishuhudiwa na mamilioni ya watazamaji, ulimwenguni kote kupitia ving’amuzi vya Dstv, Diamond aliweza kudhihirisha uwezo wake huo kwa kuangusha bonge la shoo ikiwemo kwa wimbo wake wa ‘Mawazo’ ambao uliwachanganya watu mbalimbali na kuamka vitini mwao na kupanda jukwaani na kucheza nae.
Diamond
kama kawaida yake, aliweza kuvalia vilivyo, alikonga nyoyo za
mashabiki hao kwa staili yake ya uchezaji ikiwemo ya kuigiza kama
anaanguka pamoja na ile ya miondoko ya msanii wa Orijino komed, Joti,
hadi anamaliza shoo hiyo mashabiki hao walikua na hamu ya kumuona na
kusikia nyimbo zake.
Awamu
ya pili, Mshereheshaji mkuu wa shindano hilo, Osakioduwa maalufu, IK,
aliweza kumwita tena jukwaani Diamond ilikuzungumza machache, Diamond
bila hiyana aliwashukuru mashabiki kwa sapoti waliompa na kuwapongeza
wote.
“Nimefarijika
sana,nawapendeni wote Big brother, funs, na wote” alisema Diamond na
baadae IK, alimuomba apige wimbo wa mwisho wa kufungia shoo hiyo na
kuporomosha kibao cha ‘Moyo wangu’ ambacho nacho kiliwachanganya zaidi
mashabiki huku kivutio lkikubwa kikiwa juu ya uchezaji wake huo wa
Kijoti.
Katika
shoo, hiyo, mshiriki wa Zambia, Mampi aliweza kutolewa kufuatia kupata
kura chache zilizopigwa baada ya kuingia kwenye hatari yeye na wenzake
wawili,Maneta na Lady May.
(Chanzo:http://bongoweekend.blogspot.com)
0 MAONI YAKO:
Post a Comment