June 20, 2012

 
 
Staa wa muziki wa kizazi kipya  Bongo, Naseeb Abdul  ‘Diamond  Platinumz’ amevuta mkoko wa Kijanja  wenye thamani ya ‘mkwanja wa Kibongo Milioni  60 keshi.
Akizungumza na Teentz.com  muda mfupi  baada ya  kupokea  ‘dinga’ hiyo aina ya Land Cruiser Prado TX  kutoka kwa wakala aliyekuwa akishughulikiwa  mpango mzima  wa  kuingia kwake  hapa  Bongo, Diamond  alifunguka kuwa alikuwa na mpango wa kuvuta  mkoko ‘dizaini’ hiyo kitambo lakini  kuna mambo kadhaa yakawa  yanachelewesha.
“Nashukuru Mungu kuwa  mpango wangu umetimia, nilipanga hivi kitambo lakini kuna baadhi ya mambo yalichelewesha hatua hiyo, najua watu watasenama mengi kuhusu  hili lakini ukweli ni kuwa  huu ni mchuma wangu” alisema Diamond.
Katika hatua nyingine  Diamond  alifunguka kuwa  awali alinunua  mdinga kama hiyo huko visiwani Zanzibar, lakini baada ya kuikagua aligundua kuwa lina matatizo na kuamua  kulirudisha  na kuagiza kitu kipyaaaaaa.
..Stori na Dismas Ten..



Kwa habari zaidi unaweza kucheki  ..www.thisisdiamond.com

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE