Gazeti la DAILY POST limeandika kuwa mshahara atakaokuwa
anapokea Prezzo ni dola 720,000 kwa mwaka akiwa balozi wa One Campaign.
Fedha hizo ni sawa na shilingi bilioni 1, milioni 137 na ushee za Tanzania!
Kwa mshahara huo Prezzo atakuwa akilipwa zaidi kuliko
hata viongozi wakubwa Kenya.
Mshahara wa rais Mwai Kibaki ni shilingi za Kenya
milioni 3.2 sawa na milioni 57 za Tanzania na waziri mkuu Raila Odinga akipokea
milioni 2.4 za Kenya huku Uhuru Kenyatta akipokea kama milioni 1.5 kwa mwezi.
Hii ndo payslip ya Prezzo:
Mshahara kwa mwezi : $40,000 (TSH 63,200,000)
Posho ya nyumba : $5400 (TSH 8,532,000)
Posho ya usafiri : $6600 (TSH 10,428,000)
Kuburudika: $5000 (TSH 7,900,000)
Matibabu: $10,000 (TSH 15.800,000)
Vingine: Passport
ya kidiplomasia na walinzi wawili.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment