Wiki iliyopita wasanii wa: BONGO FLEVA MKOANI MOROGORO WALIFANYA ZIARA YA PAMOJA YA KUWATEMBELEA WAGONJWA WALIOLAZWA KATIKA HOSPITAL YA MKOA WA MOROGORO.
KATIKA ZIARA HIYO AMBAYO HAIJAWAHI KUTOKEA MKOANI HAPA WASANII HAO WALITEMBELEA WORD ZOTE HUKU WAKIZUNGUMZA NA WAGONJWA WALIOLAZWA HAPO.
ZIARA HIYO ILIYORATIBIWA NA MDAU WA MZIKI HUWO SALIM CHUMA ILIWAKUSANYA WASANII NA WADAU KWA JUMLA. WASANII WALIUKUWAPO KATIKA ZIARA HIYO NI PAMOJA NA STAMINA, CRISS WAMARYA, LOTTA, MAN PRINCE NA WASANII WENGINE WENGI, WAKIWA SAMBAMBA NA PRODUCER GQ WA DIGITAL VIBES, EDDIE MASALI, AHMAD MACHAKU NA WENGINE WENGI.
BAADA YA ZIARA HIYO WASANII HAO WALIFANYA KIKAO KATIKA UKUMBI WA BWALO NA KUPANGA MAMBO YAO KWA PAMOJA, HUKU WAKIJADILI MAENDELEO Y MZIKI HUWO NA ZIARA ZINGINE AMBAYO WATAFANYA KWA PAMOJA. ALHMIS 16-8-2012 WAMEPANGA KUWATEMBELEA WATOTO YATIMA.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment