Msanii wa bongo fleva Linex Ameongea kuhusu ajali waliyoipata wakielekea
kigoma leo .Linex amesema hawakuwa kwenye mwendo wa kasi kwani show zao
ni weekend so mwendo wao ulikuwa mdogo sana na ndio maana haikuwa ajali
kubwa .Dancer mmoja wa Suma lee ameumia Mguu na Gari la Suma Lee ndio
lililoumia sana upande wa mbele,kwani taa zimepasuka na sehemu ya mbele
kuharibika sana. Ajali ilisababishwa na basi la abiria lililokuwa
katikati ya barabara kwenye kona kali, ambapo ili kulikwepa lazima Suma
angetakiwa atoke nnje ya barabara, ndipo gari ilipomshinda na kugonga
mti .Linex alikuwa sambamba na Baba levo na Suma lee ambao wana show tatu weekend hii Ijumaa
mjini Kigoma , Jumamosi ni Kasulu na Jumapili ni Bujumbura. Thank God Wako Poa.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment