Msanii Peter Mponeja a.k.a C-SIR MADINI (SISA), jana (26th
Aug 2012) ameshot video ya wimbo wake mpya kabisa ambao bado haujawa released
alioamua kuupa jina la PAIN KILLER. Video imefanywa jijini Dar es Salaam na
kampuni ya Next Level chini ya director Adam Juma.
Hii itakua ni video ya tatu
kwa msanii huyu mwenyeji wa jiji la Mwanza baada ya mbili zilizoishatangulia
kutoka ambazo ni KIFUNGO HURU aliyoitoa mwezi may 2011, pamoja na NISHIKE MKONO
aliyoitoa April mwaka huu.
Katika video hii ya Pain Killer, C-sir Madini
amevalishwa na KIDOTI FASHION ya mrembo JOKATE ambayo imeshavalisha wasanii
wengi wa bongo kama Diamond na Ommy Dimpoz kwenye video yake mpya ya Baadae.
Video ya C-sir inategemewa kuwa hewani muda wowote mwezi September
2012, na wiki moja baadea itafuatiwa na
audio katika radio stations zote.
Fuatilia picha za maandalizi na wakati wa
kushot video ya Pain Killer.
C-sir akiwa salon |
Jokate na C-sir Madini |
Location,wakati wa makeup |
![]() |
Video Model |
Dancers wakipewa maelekezo na director |
0 MAONI YAKO:
Post a Comment