October 11, 2012


Msanii wa bongo flevah nchini Tanzania maarufu kama Timbulo amesema anategemea kutoa wimbo wake mpya siku chache zijazo ambao amewashirikisha kundi la X-maleya kutoka nchini Cameroon.

Miezi kadhaa iliyopita Timbulo aliandamwa na maswali mengi yaliyoambatana na maneno ya kumshutumu kuwa ali copy na kupaste nyimbo zake mbili zilizopita "Domo Langu" na "Waleo Wakesho" kutoka katika nyimbo za kundi hilo.

Kwa mujibu wa maelezo ya Timbulo alidai kuwa haku copy bila idhini ya wenye nyimbo kama inavyodhaniwa na wengi, bali alipewa ruhusa na X-Maleya wenyewe na vithibitisho vyote anavyo.

Timbulo ameendelea kusema kutokana na kwamba anawa feel sana X-maleya na wao wanam feel, sasa ameamua kuwashirikisha kabisa katika wimbo wake mpya aliouita "Lastic ya Upendo" inayotegemewa kutoka hivi karibuni na tayari wameshamtumia demo yenye sauti zao na ya Timbulo na kinachosubiriwa sasa ni mixing imalizike.

Kupitia ukurasa wake wa facebook Timbulo leo ameandika: " Habar njema ni kwamba wimbo mpya tayar upo mkonon, waitwa Lastic ya upendo nimefanya na x-maleya, a group music from cameroun, ambao nimewah kutajwa kuiba nyimbo kutoka kwao,,,!".

Leotainment ilimuuliza Timbulo juu ya mpango wa video ya wimbo huu aliyowashirikisha wasanii kutoka nje ya Tanzania, na hiki ndicho alichojibu: 

" Wao X-maleya walitupa option tatu za kufanya video, option ya kwanza ni wao watutumie clips za parts zao walizoimba katika wimbo huu watakazo shot huko kwao. Option ya pili ni sisi tusafiri kwenda Cameroon kushot huko, na option ya tatu ni wao waje Tanzania tushot hapa. Sasa mpango mzima utafahamika mara baada ya audio ya wimbo huu kuwa released wiki ijayo kama mixing na mastering itakuwa imekamilika, lakini uamuzi wa kufanya video utatoka katika hizo option tatu".

Kazi hii ya "Lastic ya upendo"  imetengenezwa katika studio ya Combination Sound chini ya producer Man water, lakini mixing inafanyika hapa Tanzania na Cameroon kisha watachagua ile itakayokuwa nzuri zaidi kwa ajili ya official release.

Related Posts:

  • Bodaboda wezi wa simu, wakamatwa na kuchomewa pikipiki   Maeneo karibu na Ocean Road, vijana maarufu kwa ukwapuaji wa simu za mkononi wakiwa kwenye pikipiki walimkwapulia dada mmoja simu. tukio hilo lilionwa na mtu aliyekuwa kwenye gari ndipo alipoanza kuwafukuzia na k… Read More
  • Abdu Kiba awataka wasanii wa Tanzania kufanya muziki wa Live Band Ali Kiba na Abdu Kiba wakiimba kwa pamoja Ali Kiba akiimba kwa hisia katika tamsha la Sauti za Busara visiwani Zanzibar Vacalist wa Ali Kiba wakiimba kwa hisia Ali Kiba akiendeleza burudani Umati wa… Read More
  • Mkurugenzi TPA asimamishwa kazi Waziri wa Usafirishaji Samweli Sitta.  Taarigfa zilizotufiki punde zinasema kuwa Waziri wa Uchukuzi Samuel Sitta amsimamisha kazi kaimu mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya Bandari Tanzania mhandisi Madeni Kipande kutok… Read More
  • Waliowajeruhi polisi Tanga wasakwaJeshi la Polisi nchini  limesema wanawasaka watuhumiwa waliowajeruhi askari sita kwa risasi mkoani Tanga. Askari hao walijeruhiwa wakati wakifanya kazi ya kuwatafuta watuhumiwa wa uhalifu wa kutumia silaha wanaodaiwa kuw… Read More
  • CUF- Wampeleka Lipumba UKAWACUF kimesema kimepanga kulipeleka jina la Profesa Ibrahimu Lipumba ili kuomba ridhaa ya kugombea kiti cha urais. Naibu mkurugenzi wa uchaguzi wa chama cha wananchi CUF Bwana Shaweji Mketo amesema chama cha wananchi CUF kimepa… Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE