Rick Ross hapa akiwaelekeza jambo mashabiki hawapo pichani wakati alipokuwa akiimba jukwaani usiku huu.
Msanii wa miondoko ya rusha rohoo a.k.a Miduara,Shilole akijiachia jukwaani

Rick Ross akiendelea kupagawisha mashabiki wake usiku huu kwenye viwanja vya Leaders
Watu
wa usalama wakijaribu kudhibiti rapsha zilizokuwa zikijitokeza
kutokana na mashabiki wengi kuwa na hamu ya kumuona mwanamuziki Rick
Ross
Bibi Cheka na Stiko kutoka pande za TMK nao wakafanya mambo makubwa,
Wadau kutoka Serengeti wakifyurahia jambo katika burudani ya muziki.
Kulia
ni Mkurugenzi wa Masoko SBL Ephraim Mafuru na kutoka kushoto Meneja wa
Masoko SBL Emmilian Rwejuna na Mdau Rawlence Mafuru pamoja na wadau
wengine wakipozi kwa picha.
Wadau mbalimbali wakifuatilia burudani ya mwanamuziki Rick Ross wakati alipokuwa akitumbuiza,
Pichani chini na juu mashabiki wakishangilia kwa nguvu wakati wanamuziki huyo akiimba jukwaani
Rachel Mwanamuziki wa
Bongofleva kutoka kundi la THT akicheza na mmoja wa wacheza shoo wake
katika Tamasha la Serengeti Fiesta linalofanyika usiku kuu kwenye
viwanja vya Leaders jijini Dar es salaam ambapo pamoja na wasanii
mbalimbali wakali wa nyumbani, mwanamuziki maarufu wa Hiphop kutoka
nchini Marekani Rick Ross “The Boss” atahitimisha tamasha hilo kwa shoo
kali usiku huu.
Rachel na wacheza shoo wake wakiburudisha mashabiki viwanja vya Leaders jijini Dar es salaal katika tamasha la Serengeti,
RaSasa
ni zamu ya Lina wa THT akiwa jukwaani akiimba wimbo wake wa nampenda
ambao umewafanya mashabiki wa muziki kuitikia kwa nguvu wakati
akiwaimbisha hapa akipozi kwa staili ya aina yake huku akiwaimbisha
mashabiki wake
DAYNA akibenwa juujuu na wacheza shoo wake wakati akifanya vitu vyake jukwaani katika tamasha la Serengeti Fiesta 2012
Wadau kutoka kampuni ya bia ya Serengeti wakishoo love katika tamadsha hilo.
Mdau Edward na maiwaifu waki wakipozi kwa picha
Barnaba akikamua jukwaani katika tamasha la Serengeti Fiesta usiku huu.
DAYNA akimwaga mauno jukwaani wakati akiimba jukwaani usiku huu katika tamasha la Serengeti Fiesta.

Michael
Jackson wa Bongo akifanya vitu vyake mbele ya mashabiki wake alivuta
hisia za wengi kutokana na kuigiza uchezaji wa marehemu Michael Jackson
wa Marekani, pichani ni nyomi ya mashabiki waliojitokeza katika tamasha
hilo kwenye viwanja vya Leaders
Msanii Aika kutoka kundi la muziki wa Bongofleva la Per One akifanya vitu vyake jukwaani katika shoo za utangulizi
Wasanii ha wa nao wamefanya mambo makubwa katika tamasha la Serengeti Fiesta 2012 usiku huu kwenye viwanja vya Leaders.
Kutoka
kushoto ni Rachel, Lina na Daina wote kutoka THT wakiwa tayari kwa kazi
ya kuburudisha mashabiki wa Tamasha la Serengeti Fiesa 2012.
Umakini kubwa kutoka kwa mashabiki kama wanavyoonekana katika picha
Mashabiki wakidatishwa na burudani za mwanzo za tamasha la Serengeti Fiesta usiku huu kwenye viwanja vya Leaders.
Msanii Aika kutoka kundi la Per One akifanya vitu vyake jukwaani na wasanii wenzake.
Jeshi la polisi nalo lilikuw amakini sana katika shoo hiyo.

0 MAONI YAKO:
Post a Comment