October 10, 2012

Hiki kinaweza kuwa kituko cha mwaka kwenye muziki wa Bongo Flava. Mrembo aliyeigiza kwenye video ya Linex Aifola, ameamua kumfungulia RB msanii huyo baada ya kumpiga kibao cha kweli kwenye video hiyo.

Katika video hiyo Linex anaonekana akiwa amekaa kwenye kochi na kuanza kukagua simu ya mchumba wake Aifola ambaye humo ameigiza Janeth Bundala na ndipo alipogundua kuna meseji za kimapenzi anazotumiwa na mwanaume mwingine kiasi cha kuchukia na kumpiga kofi kali la shavuni.
hahhahahahhahaha frm no where eti janeti aka aifola kanipigia leo kaniambia kanichukulia R B kwa kofi nililompiga wakati tunaigiza hahah kama kachelewa hv,” aliandika Linex jana kupitia Facebook.
“Sijajua alikua anatania but ndo kitu alichoniambia muda si mrefu nimekia nacheka tu. Nimemsikia live radion anataka kulipwa aseeee kumbe anamaanisha. Nimeshaongea nae na kesho ndo nakutana nae rasmi ntajua anatakaje na ntamalizana nae.”

Unahisi Janeth yuko sahihi kumshtaki Linex kwa kumpiga kibao cha kweli kwenye uigizaji wa video? Na je amechelewa kama Linex anavyosema?

Related Posts:

  • Shambulizi la uhalifu wa mtandao laathiri mataifa 99 duniani   Sambulizi la kihalifu mitandaoni lililotendeka kupitia utumizi wa vifaa vinavyoaminika kuibwa kutoka kitengo cha ujasusi nchini Marekani NSA limeathiri mashirika tofauti duniani. Kampuni ya kulinda uhalifu wa mi… Read More
  • Shambulizi la komputa kuathiri watu zaidi Jumatatu   Wataalmu wa usalama katika mitandao ya komputa, wanaonya kwamba kunaweza kutokea mashambulio mengine sehemu mbalimbali za dunia, pale watu wataporudi makazini hapo kesho. Inakisiwa kuwa komputa zaidi ya 120 kat… Read More
  • Ashikiliwa na Polisi kwa kumuua mumewe kisa wivu   MKAZI wa Wilaya ya Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba, Khadija Mbarouk (44), anashikiliwa na polisi kwa madai ya kumuua mumewe kwa sababu zilizoelezwa kuwa ni wivu wa kimapenzi. Mtuhumiwa huyo inadaiwa alimchom… Read More
  • Rais mpya wa Ufaransa aapishwa   Rais mpya wa Ufaransa, Emmanuel Macron, anaapishwa hivi sasa, juma moja baada ya kupata ushindi mkubwa katika marudio ya uchaguzi mkuu wa Urais nchini humo. Alimshinda pakubwa kiongozi wa chama cha kulia Bi Marin… Read More
  • TRA Wakana kuhsu Ml 400 za Diamond Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania, (TRA), Bw. Richard Kayombo (katikati), akitoa hotuba ya ufunguzi wa semina ya siku moja ya ujasiriamali na elimu ya kulipa kodi kwa waandi… Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE