
Mkali wa muziki wa kizazi kipya nchini toka mkoani Tanga Joseph Lushahu 'Bwana
misosi'Ameamua kuvuta pumzi kwa kuamua kuimba kwa mtindo wa Rhumba
Bwana Misosi amefunguka kuwa siku si nyingi anataraji kuachia ngoma yake mpya inayoitwa 'Iweje' iliyofanyika katika studio za jiko(Studio) la Hm Records iliyopo Kawe
"Si kama nitaacha kuimba bongo fleva moja kwa moja, nimeamua kupiga Rhumba kwa sababu ni moja ya style ambazo zipo kwenye muziki na watu
wanazifanya wanatusua soo, baada ya ngoma kutoka kitafuatia kichupa
ambacho pia kitanyongwa hapo hapo Hm". alisema Bwana Misosi akizungumzia kuhusu hilo.
Chanzo: baba jonii
0 MAONI YAKO:
Post a Comment